Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za bianadamu na watu, Imani Aboud watano kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa nchi mwanachama wa mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu leo  Novemba 8, 2021 jijini Dar es Salaam.
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za bianadamu na watu, Imani Aboud akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kufungua kikao cha 63 kitakachodumu kwa mwezi mmoja.

MAHAKAMA ya Afrika ya haki za binadamu na watu imeanza kikao cha 63 cha majaji kwa ajili ya kusikiliza mashauri 15 yaliyowasilishwa katika mahakamani hiyo.

Katika kikao hicho kilichoanza leo Novemba 8,2021 kitadumu kwa muda wa mwezi mmoja mpaka Desemba 2, kinaendeshwa na jopo la majaji 11 kutoka nchi mbalimbali wanachama ambapo watatoa hukumu ya mashauri hayo.

Akizungumzia mashuri hayo yanayoendelea kusikilizwa Rais wa Mahakama hiyo, Iman Aboud, amesema katika mashauri hayo asilimia 70 yanatoka nchini Tanzania.

Aidha Rais Imani amewapongeza majaji wa Mahakama hiyo kwa mchango wanaoutoa katika kushughulikia mashauri na kutoa maamuzi.

"Sababu kwanini majaji wanastahili pongezi ni kutokana na uwajibikaji wao na ujasiri sifa zinazotakiwa kwa kila mtu na taasisi ili kupima uwezo wake," amesema Aboud

Rais Aboud pia amewahakikishia majaji pamoja na wafanyakazi wa Mahakama hiyo ya Afrika kuwa Mahakama hiyo itaendelea kuwepo na kuendelea na shughuli zake kama kawaida licha ya kwamba inakabiliwa na wakati mgumu kwa wadau wake kusitasita na kuwepo kwa upungufu wa rasilimali kutokana na ushirikiano unayopata inaweza kukabiliana na changamoto hizo.

Ametolea mfano ushirikiano ambao Mahakama hiyo inaendelea kupata kuwa ni kitendo cha nchi mbili kujiunga uanachama wiki iliyopita ambazo ni Niger na Guinea Bissau.

Ameongeza kuwa, pamoja na kwamba wanafahamu changamoto walizopata kutoka kwa nchi wanachama ambazo ni Benin, Ivory Coast na Tanzania lakini leo tena amewakaribisha wazungumzie maeneo chanya waliyonufaika nayo kupitia nchi hizo.

Amesema, siku zote mwanzo ni mgumu na kwamba tayari Mahakama hiyo inapata ushirikiano mzuri na Benin na kuziomba nchi nyingine kujiunga katika mazungumzo ya mabadiliko ndani ya Mahakama hiyo.

Majaji hao 11 ni kutoka nchini Tanzania, Congo Brazavile, Kenya, Tunisia, Cameroon, Nigeria, Algeria, Malawi, Mali, Afrika ya Kusini na Rwanda.
Majaji wa nchi mwanachama wa mahakama ya Afrika ya Haki za binamu na watu wakiwa katika kikao cha wa 63 kwaajili kujadili mashauri yaliyowasilishwa mahakamani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...