Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano wake na taasisi pamoja na mashirika yote yenye nia kushirkiana na Serikali katika kuwaletea huduma wananchi wake.

Mhe. Hemed ameeleza hayo wakati akizungumza na viongozi wa Shirika la Kimataifa la maendeleo Duniani, linalosaidia kutoa huduma za kuwafikia watu wenye ulemavu Duniani (CBM) waliofika Afisini kwake Vuga jijini Zanzibar.

Amesema Zanzibar kuna uhitaji mkubwa wa huduma mbali mbali kwa wananchi wake, hivyo ujio wa Shirika hilo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia wananchi, na kuwapatia huduma ikiwemo matibabu ya macho sambamba na kuwasaidia watu wenye ulemavu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa, Serikali haina pingamizi yoyote juu ya utekelezaji wa huduma zinzotolewa na CBM, na ameuagiza uongozi wa Wiara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto, kuhakikisha mpango huo unaanza haraka utekelezaji wake kwa kutoa huduma kwa jamii.

Nae, Mkurugenzi mkaazi wa shirika la CBM Nesia Mahange amesmea shirika lao limeamua kuunga mkono jitihada za serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na uhitaji mkubwa uliopo wa huduma za macho pamoja na masuala mbali mbali ya kijamii yanayohusu mambo ya kimaendeleo.

Mkurugenzi Nesia ameleza kuwa shirika la CBM lina zaidi ya miaka Hamsini (50) tangu kuanzishwa kwake na linatoa huduma za rasilimali fedha,utaalamu, kujenga miundombinu, kutoa elimu jumuishi na kusomesha wataalamu kupitia sekta ya Afya ya macho, Elimu Jumuishi, Makaazi pamoja misaada ya huduma za kibinadamu itokanayo na masuala ya maafa.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiuthibitishia Uongozi wa Shirika la kimataifa la maendeleo duniani linalosaidia kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu (CBM) kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kushirkiana na mashirika yalionesha nia ya kuwasaidia wananchi wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...