WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Kitila Mkumbo ameshiriki Kongamano la Nne la Kimataifa la mauzo ya ndani lililofanyika Shanghai nchini China na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali duniani kwa njia ya mtandao

Kongamano hilo limefunguliwa Leo tar. 4 Novemba, 2021 na Mhe. Xi Jimping Rais wa Jamhuri ya watu wa China ambapo katika hotuba yake ameeleza namna nchi ya China inavyotoa mkazo katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa hususan katika eneo la biashara chini ya mifumo ya kitaasisi ya dunia kama vile Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Aidha Mhe. Xi Jimping amewahakikishia nchi marafiki ambao wanafanya biashara na China kuwa serikali yake itaendelea kufungua zaidi milango ya masoko yake kwa bidhaa zitakazozalishwa katika nchi hizo na zinazohitajika kwa wingi nchini China.

Viongozi wengine walioshiriki na kutoa hotuba kwa njia ya mtandao katika kongamano hilo ni pamoja na Rais wa Argentina, Kazakhstan, Zambia, Waziri Mkuu wa Italia, Thailand, Kaimu Waziri Mkuu wa Fiji.

Viongozi wengine walioshiriki ni pamoja na Mhe. Ngozi Okonjo Tweala Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) pamoja na Mhe. Rebecca Grynspan Katibu Mtendaji wa UNCTAD.

China na Tanzania zina mahusiano mazuri ya kibiashara ambapo kwa mujibu wa takwimu za mauzo za mwaka 2020 kupitia Mamlaka ya Maendeleo Biashara Tanzania (TanTrade) jumla ya thamani ya biashara baina ya nchi hizi mbili ilikuwa Shilingi Trilioni 5.9 ambapo nchi ya China imeuza zaidi bidhaa za viwandani na Tanzania imepeleka zaidi bidhaa za Kilimo, mifugo, misitu na Madini nchini China.

Nchi zote washiriki katika Kongamano hili wamepewa fursa ya kuonesha bidhaa na huduma zao kupitia Banda la kimtandao (Virtual Pavilion) ambapo Tanzania ilionesha bidhaa za mazao zilizoongezewa thamani Kama vile kahawa, korosho, chai, viungo, asali; vivutio vya utalii na utamaduni pamoja na fursa za uwekezaji katika miradi mikubwa ya kimkakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...