Chanjo za COVID-19 zinaufundisha mwili wako jinsi ya kupambana na virusi vinavyokufanya uugue. Chanjo za COVID-19 (sindano) hazitakupa ugonjwa huo. Chanjo huufanya mwili wako ufikirie kwamba una ugonjwa na kujiweka tayari kupambana nao bila kuupata. 

Chanjo itakusaidia usipate maradhi iwapo utakuwa katika hatari ya maambukizi ya virusi vya korona. Chanjo ni salama na zenye ufanisi. 

Chanjo zote zilipitia majaribio ya kiafya kabla hazijakubaliwa kutumika kwa dharura. Watafiti walikuwa wakishughulika na chanjo za virusi vingine vya korona kwa miongo kadhaa. Chanjo zote ni salama na zina ufanisi sawa katika kuzuia kulazwa hospitalini na kifo. Hata ukipatwa na Corona huwezi kuwa mahututi wa kuwekewa gesi tofauti na asiyechanja. Yaani hutokuwa hoi taabani ukiwa umechanjwa

Hiki ndicho kiwango cha kawaida kinachotumika kutathmini chanjo zingine kama vile chanjo dhidi ya mafua. Hazina maikrochipu, tishu za fetasi, bidhaa za nguruwe, mayai, gelatini, mpira au vihifadhi. 

 Watu wengi walio na matatizo ya kimatibabu pia wanapaswa kupata chanjo. Watu walio na baadhi ya matatizo wana uwezekano wa kuugua sana ikiwa watapata COVID-19, kwa hivyo hatua ya kupata chanjo inaweza kuwa muhimu zaidi. Ikiwa huna uhakika iwapo unapaswa kupata chanjo, zungumza na mtoa huduma wako wa afya. 

 Athari zinamaanisha chanjo inafanya kazi. Unaweza kupata athari baada ya kupata chanjo ya COVID-19. Hii ni kawaida na ndivyo mwili wako unavyojifunza kupambana na COVID-19. Watu wengine hawana athari zozote. Athari za kawaida ni:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...