Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza katika Uzinduzi wa kituo Cha Afya kipya kilichofunguliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Marie stopes kilichohamia Mtaa wa Ghana Mkabala na Rock City Mall jijini Mwanza.

SHIRIKA lisilo la Kiserikali Marie stopes linaloshughulikia Afya hususani Afya ya uzazi na kwa ujumla imezindua kituo kipya cha Afya Mtaa wa Ghana Mkabala na Rock City Mall jijini Mwanza.

Aidha, Shirika Hilo la Marie stopes limekua likishirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,jinsia,Wanawake na watoto kupitia tawala za Mikoa na Serikali za mitaa katika kufikia jamii kwa elimu na huduma ya Afya ya uzazi na Afya kwa ujumla katika Mikoa mbalimbali nchini.

Katika kuunga Mkono juhudi za Serikali Shirika Hilo ina Zahanati 9 katika Mikoa ya Unguja, Zanzibar,Musoma,Kahama,Mwanza,Mbeya,Iringa,Kimara,Arusha na hivi karibuni kituo cha Afya kitafunguliwa Makambako.

Shirika Hilo kwa kuboresha huduma zao wamefungua kituo cha Afya kilichokua Nyegezi Mkabala na kituo cha Mabasi na kwa Sasa kituo hicho kimehamia Mtaa wa Ghana Mkabala na Rock City Mall jijini Mwanza.

Pia wemewakaribisha wateja waliokatibu na Makazi hayo mapya na kuwahaidi wateja wao kupata huduma bora kutokana na kuboresha wigo kwa upande wa wataalamu na hivi karibuni kutakuwepo daktari bingwa wa watoto na daktari bingwa wa akina Mama ambao watakua wakitoa huduma kwenye kituo hicho.

Pia huduma zingine zitakazopatikana ni vipimo vya ultrasound,vipimo vya maabara,uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi pamoja na chanjo wahoma ya ini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...