Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza S. Johari amefungua mkutano wa 41 wa mwaka wa chama cha waongozoji ndege Tanzania (TATCA). 

Mkutano huo umefanyika leo Novemba 26, 2021 Peacock Hotel na kuhudhuriwa na wajumbe wa TATCA, Rais wa TATCA Bw. Shukuru Nziku, Rais wa Chama cha Waongozaji Ndege Kenya (KATCA) Bi. Maureen Isika, Rais wa Chama cha Waongozaji Ndege Uganda (UGATCA) Bw. Tonny Kepler Ssenkubuge, Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, wawakilishi wa vyama vingine vya usafiri wa anga Tanzania (TAISOA na TATSEA) pamoja na mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUGHE Bi. Jackline Ngoda.

Bw. Johari amesema kuwa, Mamlaka inatambua kwamba waongozaji ndege pamoja na kada nyingine wanahitaji kupewa mafunzo yatakayozidi kuwajengea uwezo wa utendaji na utekelezaji wa majukumu yao na hivyo Mamlaka hiyo itahakikisha inawapatia wataalam hao mafunzo thabiti yatakayoongeza weledi katika maeneo yao ya kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akizungumza na wataamu wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) kuhusu namna Mamlaka ilivyojipanga kuwawezesha Waongozaji ndege kufanya kazi kwa weledi na ufanisi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 41 wa mwaka  uliofanyika leo Novemba 26, 2021 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Shukuru Nziku akizungumza kuhusu jinsi chama hicho kilivyoweza kuwasimamia pamoja na kuwapatia elimu waongoza ndege nchini Tanzania wakati wa kufunguzi wa Mkutano wa 41 wa TATCA uliofunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari leo Novemba 26, 2021 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akitoa neno kwenye mkutano Mkutano wa 41 wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) uliofanyika leo Novemba 26, 2021.
Mwenyekiti Mpya wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Jackline Ngoda akitoa hamasa kwa wanachama wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) kujiunga na na TUGHE tawi la TCAA wakati wa mkutano mkuu wa 41 uliofunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari leo Novemba 26, 2021 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Godlove Longole akizungumza jambo kwenye mkutano wa 41 wa mwaka wa TATCA leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wataalam wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), viongozi wa TCAA wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari(hayupo pichani) alipokuwa anafungua mkutano mkuu wa 41 wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) uliofanyika leo Novemba 26, 2021 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari(aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waongoza ndege Tanzania waliohudhuria mkutano wa 41 wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) uliofanyika leo Novemba 26, 2021 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna waongoza ndege wanavyotakiwa kupewa elimu kila wakati ili kuendana na teknolojia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 41 wa mwaka  uliofanyika leo Novemba 26, 2021 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Shukuru Nziku akizungumza na wandishi wa habari kuhusu malengo ya chama hicho ikiwa ni kuwaweka wanachama pamoja ili kuendana na wakati pamoja na kuwapa mafunzo wanachama hao kwenye mafunzo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 41 wa mwaka  uliofanyika leo Novemba 26, 2021 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...