Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka ametembelea fukwe za Coco kujionea hali
ya ujenzi wa vibanda vya biashara na
kuangalia changamoto mbalimbali za kimazingira katika eneo hilo.
Amesema kuwa kuna athari mbalimbali za kimazingira ambazo
zimeonekana katika ujenzi huo unaoendelea mahala hapo ambazo zimesababishwa na
shughuli za kibinadamu zilizoko katika eneo hilo. “Serikali inawajibika kulinda mazingira
hususan kwenye maeneo ya fukwe ambazo kwa sasa tunaona zinaathirika sana na
shughuli za kibinadamu, wote mmeona
jinsi ambavyo kingo za bahari zinaliwa sababu ya changamoto ya mabadiliko ya
tabianchi”
Akiongeza amesema kuwa Manispaa ya Kinondoni ndiyo wanasimamia eneo hilo na wanatakiwa kufuata utaratibu wa Athari za Tathmini ya Mazingira (TAM) kwani kuna athari za wazi kabisa amabazo zimeonekana ikiwepo suala la utupaji wa taka ngumu katika maeneo hayo ya fukwe. Je, mfumo unakuaje na mfumo wa maji taka katika eneo kama hilo lenye watu wengi ukoje? .
“Unapokuwa na idadi kubwa ya watu katika eneo hili lazima kuwa na sehemu za utupaji taka ngumu na mfumo wa maji taka yaani vyoo na usalama wao kwa ujumla watu wanapokuwa hapa unakuaje? wote mmeona mawe yenye ncha kali yako pembezoni mwa vibanda hivi vya biashara ”. Amemaliza kwa kusema kuwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa miradi kama hiyo ni muhimu kwani nia na madhumuni ni kujiridhisha na mambo makubwa ya msingi ambayo yanaboresha afya na ustawi wa yule atakayepata huduma katika vibanda hivyo vya fuke za coco.
“ Hatuangalii tu faida ya yule mjasiriamali wala faida ya yule anayewekeza
kuuza bidhaa mbalimbali bali tunaangalia pia
kwa mkazi anayekuja kufurahia hapa afya yake, usalama wake vikoje? Lakini pia ndani ya eneo hili la mita 60 ni
haki ya kila mwananchi kukaa katika
eneo hili na akawa salama, je
ustawi wa mazingira ukoje na waliojenga hivi vibanda wanawajibika vipi
kuhakikisha kuwa kuna usalama lakini pia mabadiliko ya tabia nchi yanadhibitiwa
ili athari tunazoziona zisiendelee
kuwepo yote hayo ni mambo ya Msingi tunayopaswa kuyafahamu kabla
hatujaingia kuanza kuweka mradi wowote katika maeneo ya fukwe kama tunavyoona
hapa coco alimalizia Dkt. Gwamaka”.
Baada ya kumaliza ziara hiyo Mkurugenzi Gwamaka aliahidi kuwasiliana na Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa, Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondoni pamoja na TAMISEMI na kuona ambavyo kwa pamoja wataweza kurekebisha
na kuboresha yale ambayo walikua wamekusudiwa
kuyafanya katika eneo hilo la fukwe za coco.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...