PATRICIA KIMELEMETA

MKURUGENZI Mtendaji wa Kiwanda cha Woiso Original Product, Kenneth Woiso amewashauri watanzanua kununua bidhaa zinazozalishwa nchini kwa sababu zina ubora kuliko bidhaa zinazotoka nje ya nchi na kuuzwa kwa gharama nafuu.

Akizungumza hivi karibuni, Woiso alisema kuwa, viatu vinavyotengenezwa nchini vinatumia ngozi origino ambayo inazalishwa hapa nchini, lakini viatu vinavyoyoka nje ya nchi, baadhi yao vinatumia ngozi ghushi iliyochangwa na plastiki.

Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, watanzania wanapaswa kupewa elimu ili waweze kutofautisha kati ya ngozi ghushi na ngozi origano hata wanapoenda dukani wanachagua kitu bora ambacho kimetengenezwa kwa ngozi origino.

"Watanzania wengi wanapenda kununua bidhaa zilizotengenezwa nje ya nchi wakiamini kuwa ni bora zaidi kuliko bidhaa zinazotrngenezwa ndani ya nchi, wakati sio kweli, bidhaa zetu ni bora na zinatrngrnezwa kwa kiwango cha juu kwa kutumia ngozi originao na sio ngozi ghushi," alisema Wosio.

Aliongeza kuwa, ndomana bidhaa za nje ya nchi zinauzwa bei nafuu ili kuvutia wateja kwa sababu haziwezi kudumu muda mrefu kutokana na ubora wa kiwango cha chini.

Alisema kuwa, hivyo basi wakati umefika wa Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutoa elimu kwa wananchi waweze kutambua ubora wa bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchi na kutofautisha na bidhaa za ngozi zinazotoka nje ya nchi

Alisema kuwa, viatu anavyotengeneza ananunua ngozi kutoka kwenye viwanda vya ndani ya nchi vinavyotengrneza bidhaa hizo, jambo ambalo limesaidia kuwa na viatu bora vinavyodumu muda mrefu kuliko vile vya nje.

"Nanunua ngozi kutoka kwenye viwanda vya hapa nchini ambavyo na vyenyewe vinanunua ngozi kutoka kwa wafugaji na kupeleka kiwandani kwa ajili ya kuiboresha na kutuuzia,ndomana viatu vyetu vinakaa muda mrefu kutoka viatu vinavyotoka nje ya nchi zenye majina makubwa," alisema.

Alisema mpaka sasa, bidhaa zinazozalishwa kwenye Kiwanda hicho zinauzwa katika nchi mbalimbali zikiwamo za Afrika Mashariki na Dubai, hali ambayo imesaidia kukuza soko la nje na kuitangaza nchi kibiashara.

Alisema kuwa, mkakati uliopo ni kuendelea kutoka elimu kwa wananchi Iwaweze kutofautisha kati ya ngozi bora na ngozi ghushi, jambo ambalo litasaidia kuongeza mauzo kwenye soko la ndani na serikali kupata mapato.

"Kuna baadhi ya nchi maarufu wanatengeneza bidhaa za ngozi ghushi na kuzileta nchi, tena zinauzwa kwa bei nafuu na wateja wanakimbilia, lakini hazidumu muda mrefu kwa sababu zimetengenezwa chini ya kiwango," alisema.

Kiwanda cha Woiso kunazalisha bidhaa mbalimbali zikiwamo viatu, mapazia, samani za ndani na magodoro.

Waziri wa Kiwanda na Biashara,Profesa Kitila Mkumbo alisema kuwa, ngozi zinazozalishwa nchini zina kiwango bora na kukidhi masoko ya ndani na nje ya nchi na kuwataka wananchi kupenda kununua bidhaa za ngozi za ndani ambazo ni origino zinadumu muda mrefu.

"Tumejitahidi sana kuboresha ngozi zetu kutoka kwa wafugaji hadi kiwandani, jambo ambalo limesaidia kupata masoko ya ngozi ya ndani na nje ya nchi.

Alisema mpaka sasa kuna viwanda vikubwa vitano vya kutengrneza ngozi na viwanda vidogo vidogo ambavyo vinazalisha ngozi bora inayokidhi matakwa ya sheria ya bidhaa za ngozi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...