Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi amefanya ziara katika Mradi wa kuzalisha vifaa vya Umeme (Electrical Products) wa Kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD na kupokelewa na meneja wa mradi huo Dkt. Ibrahimu Qamar maeneo ya Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni leo tarehe 25 Novemba, 2021.
Nae Dkt. Ibrahimu amesema kwa sasa kampuni ipo kwenye hatua za mwisho za ufungaji wa mashine 15 walizopokea na kukamilisha ujenzi.
Wakati huohuo Dkt. Maduhu ametembelea eneo la mradi wa INDUSTRIAL PARK lililipo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni ambapo kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD itatekeleza uwekezaji huo.
Dkt. Maduhu amewapongeza kwa hatua nzuri waliyofikia na amewaeleza kuwa kama kutakuwa na changomoto zozote kwenye kutekeleza mradi wao wasisite kuziwasilisha TIC kwa ajili ya kuzitatua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi, wa pili kulia, akipatiwa maelezo na Meneja mradi Dkt. Ibrahimu Qamar katika Mradi wa kuzalisha vifaa vya Umeme (Electrical Products) wa Kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD uliopo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni leo tarehe 25 Novemba, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi, wa pili kutoka kushoto, akipatiwa maelezo na msimamizi wa mradi Bw. Mahmoud Abobakar, wa kwanza kushoto, kuhusu maendeleo ya mradi alipotembelea eneo la INDUSTRIAL PARK lililipo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni, ambapo kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD itatekeleza uwekezaji huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi na wafanyakazi wa mradi wa kuzalisha vifaa vya Umeme (Electrical Products) wa Kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD uliopo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni leo tarehe 25 Novemba, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi, alipotembelea eneo la INDUSTRIAL PARK lililipo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni, ambapo kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD itatekeleza uwekezaji huo leo 25 Novemba, 2021.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...