Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandis Marwa Rubirya amewataka wahandisi wa TANROADS na TARURA kukamilisha taratibu za manunuzi ili kutengeneza barabara zilizopo kwenye halmashauri kwa wakati.
Mhandisi Rubirya amesema hali ya matengenezo hairidhishi na kuagiza Tanroads na Tarula kuanza mapema mchakato wa manunuzi kabla mvua hazijaanza.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandis Rubirya ametoa kauli hiyo akiwa katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe na kutaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa miundombinu ya barabara.
“Tunaelekea mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja lakini bado haliridhishi lakini kama mvua ingeanza kunysha hali ingekuwa ni mbaya zaidi kwa hiyo ni lazima mbadilike,mchakato wa manunuzi uanze mapema ili wandarasi wapatikane kwa wakati na hatimaye matengenezo yaanze kabla ya msimu wa mvua”alisema Rubirya
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha bodi ya barabara akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Valentino hongoli na mbunge wa makambako Deo Sanga wametaka serikali kuharakisha matengenezo ya barabara ya Kibena Madeke hadi Mlimba kwa kiwango cha lami.
“Lakini kuhusu barabara ya Kibena-Lupembe ushauri wangu kwasababu kuna fedha ambazo zilishatengwa tungeanza hata kama hela ni kidogo”alisema Deo Sanga Mbunge wa Makambako
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe Bwana Jasel Mwamwala amesema barabara ya Kibena Madeke hadi mlimba inatakiwa kutiliwa mkazo kwani kisiasa italeta athali kwa chama.
“Katika kikao kilichopita tulionyesha kwamba barabara hii ya Njombe-Lupembe inaweza ikatughalimu tulieleza kabisa ianze kujengwa na tukizungumzia kisiasa tutapata shida kweli kweli uchaguzi ukija kwasababu tuliahidi,mimi nafikiri hebu tutizame ili tusijekuathirika”alisema Mwamwala.
Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akizungumza na wajumbe wa kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Njombe kilichofanyika hii leo katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha bodi ya barabara wakisikiliza michango mbali mbali juu ya ujenzi wa miundombinu na utekelezaji wake unaoendelea mkoani Njombe.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...