Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Joseph Sokoine katika kikao cha 15 cha Maafisa waandamizi kutoka nchi za
Afrika na China wakati wa kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha
Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC)
kilichofanyika tarehe 28 Novemba ,2021 jijini Dakar nchini Senegal.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Joseph Sokoine akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha maandalizi
ya Kikao cha Nane cha Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na
Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar
nchini Senegal .
Wajumbe
kutoka nchi mbalimbali za Afrika katika kikao cha maandalizi ya Kikao
cha Nane cha Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika
(FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar nchini
Senegal .
Washiriki
wa kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha Mawaziri wa Jukwaa la
Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28
Novemba, 2021 jijini Dakar nchini Senegal wakifuatilia kikao hicho .
Washiriki
wa kikao cha maandalizi ya Kikao cha Nane cha Mawaziri wa Jukwaa la
Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28
Novemba, 2021 jijini Dakar nchini Senegal wakifuatilia kikao hicho .
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine (katikati) baada
ya kumalizika kwa kikao cha maafisa waandamizi kwa ajili ya maandalizi
ya Kikao cha Nane cha Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na
Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 28 Novemba, 2021 jijini Dakar
nchini Senegal .
Na mwandishi wetu, Dakar
Mkutano
wa Nane wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika
(FOCAC) unaanza leo tarehe 29 hadi 30 Novemba 2021 jijini Dakar nchini
Senegal.
Maafisa
waandamizi kutoka katika nchi za Afrika na Jamhuri ya Watu wa China
wamekamilisha maandalizi yaliyokuwa yanahitajika ya mkutano huo, kwa
kupitia na kukubaliana na nyaraka za taarifa za utekelezaji wa miaka
mitatu baada ya kikao cha saba katika kikao kilichofayika tarehe 28
Novemba, 2021.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Joseph Sokoine ameongoza ujumbe wa Tanzania hicho, ambacho pia
kilihudhuduriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mpango Zanzibar
Dkt. Juma Akil, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bibi Amina
Shaaban, Balozi wa Tanzania Nigeria ambaye pia anaiwakilisha Tanzania
nchni Senegal Dkt. Benson Bana na Balozi Ceasar Waitara Mkurugenzi wa
Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkutano
huo wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika,
utakuwa chini ya Wenyekiti Wenza wa Rais wa Jamhuri ya Senegal Mhe.
Macky Sall na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping ambao pia
watahutubia wakati wa ufunguzi wake.
Mkutano
huo unatarajiwa kufanya maamuzi na kutoa maelekezo kuhusu utekeleaji wa
masuala ya namna ya kuendelea kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa
Korona, ushirikiano kati ya China na Afrika, Ushirikiano wa Kisiasa,
Ushirikiano wa Kiuchumi, Ushirikiano wa Maendeleo ya Kijamii, Utamaduni
na Ushirikiano kati ya Watu na Watu, Ushirikiano wa Ulinzi na Usalama,
Mapinduzi ya Kijani, Ubadilishanaji Uzoefu katika masuala ya Uongozi
Bora pamoja na Maendeleo ya Kitaasisi ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya
China na Afrika na mabadiliko ya tabia nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...