Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wengine
limefanikiwa kudhibiti mauaji ya albino na vikongwe baada ya kuanza
kutoa elimu sahihi kwa waganga wa tiba asili kuhusu madhara ya ramli
chonganishi.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi George
Kyando amesema baada ya kubaini kuwa vifo vya albino na vikongwe
vinachangiwa na ramli chonganishi, Jeshi hilo kwa kushirikiana na wadau
wengine lilijikita kwenye utoaji wa elimu sahihi kwa waganga wa tiba
asili.
Amesema
ramli chonganishi ilikuwa inachochea chuki miongoni mwa wananchi hivyo
kusababisha mauaji kwa vikongwe kutokana na visasi na imani potofu .
“Tulifanya
sensa na tukawashauri waunde uongozi ili waganga wote wajisajili na
tukigundua kunamauaji yametokewa ni imani za kishirikina waganga wote wa
eneo hilo wanapatashida sisi kitengo cha Polisi jamii kinapita kutoa
elimu kwamba waganga wote wajiepushe na imani za kishirikina mtu akija
kwako wewe mpe dawa, mtibu tu kumwambia aliyefanya hivi ni fulani huo ni
uchonganishi”.
Kamanda
Kyando ameonya waganga watakaobainika kukiuka maelekezo ya serikali
watafungiwa vibali vyao na kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Sisi
hatuna ugomvi na hatupingi tiba asili lakini epukeni kutoa ramli
chonganishi shughulikeni na ugonjwa na mganga yeyote tutakea mbaini mkoa
huu ambaye anajihusisha na hizo ramli tutamuondoa kwenye hiyo biashara
akafanye kazi nyingine”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...