JESHI la Polisi nchini limeipongeza kampuni kongwe ya ulinzi ya SGA Security kwa kuzingatia viwango na weledi wakati wa kuajiri walinzi wapya wa kampuni hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kawe, SP Suphian Kasanga, wakati wa akitoa salamu za jeshi hilo kwenye hafla ya gwaride la wahitimu 50 wa kampuni ya SGA baada ya kupata mafunzo ya mwezi mmoja yaliyofanyika katika chuo cha mafunzo cha SGA kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
SP Kasanga alisema kuwa umakini wa kampuni ya SGA katika kuajiri wafanyakazi wake umedhihirishwa na elimu za wahitimu hao 50, ambao alisema 11 wana shahada ya kwanza ya chuo kikuu kila mmoja, 13 wengine wana vyeti za stashahada na vyeti vya awali na waliosalia ni wahitimu wenye elimu ya kidato cha nne au cha sita.
Aidha SP Kasanga aliipongeza kampuni hiyo kwa kuajiri walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo na wale waliopitia jeshi la kujenga Taifa, jmabo ambalo alisema linaonyesha ni jinsi gani kampuni hiyo inavyozingatia umakini katika kuajiri kwake.
"SGA ni miongoni mwa makampuni machache ambayo yako makini wakati wa zoezi la kuajiri kwa kufuatilia historia ya wanaoomba nafasi za kazi pamoja na kuchukua alama za vidole vya wanaoajiriwa na kampuni hiyo kama inavyoelekezwa na mamlaka za serikali”, alisema.
Mkuu huyo wa kituo alitoa wito kwa makampuni mengine ya ulinzi kuiga mfano wa kampuni hiyo jambo amalo alisema litaepusha uajiri wa watu wasiokuwa na sifa katika sekta ya ulinzi hapa nchini.
SP Kasanga pia aliipongeza kampuni ya SGA kwa kuzingatia uwiano wa jinsia wakati wa kuajiri kwake kutokana na idadi kubwa ya waliohitimu siku hiyo kuwa wanawake na ambao alisema walifanya vizuri jambo ambalo alisema limedhihirishwa na tuzo mbalimbali walizopokea kutokana na kufanya vizuri kwenye mafunzo hayo.
"Uamuzi wenu wa kukubali kuajiri wanawake na wakajitokeza kwa wingi huu na zaidi ya yote wakafanya vyema kwenye mafunzo yao, kunadhihirisha wazi ya ukwa kuna nafasi za ajira kwa wanawake kwenye makampuni ya ulinzi ya kibinafsi”, alisema.
Mbali na kutoa pongezi kwa wahitimu hao na uongozi wa kampuni ya SGA, SP Kasanga alitoa ushauri kwa wahitimu watakaopewa majukumu ya kutumia silaha za moto kuhakikisha wanakuwa makini wakati wakiwa kazini, ambapo alisema wahalifu wengi hulenga kuwavamia walinzi wenye silaha na kuwapora silaha hizo na kisha kwenda kuzitumia kufanyia uhalifu.
Aliwashauri maafisa hao kuwa waangalifu na kuepuka vishawishi kama vile vya chakula wanavyopewa wawapo kazini pamoja na pombe kutokana na kile alichoeleza ya kwa wahalifu wengi hutumia mbinu hizo kwa kuwawekea dawa za kulevya na kisha kuwapora silaha.
Aidha aliwaonya wahitimu hao kuepuka tabia mbaya zile za kutoa sare za kazi na silaha kwa wahalifu, matumizi mabaya ya simu wakati wa kazi pamoja na kutoa taarifa kwa wahalifu ili wafanikishe uhalifu kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaenda kinyume cha maadili ya usalama.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mendaji wa kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania Bw.Eric Sambu, alieleza kuwa kampuni hiyo imejikita zaidi katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na kwamba ili kutekeleza azma hiyo imetumia na inaendelea kutumia raslimali nyingi lengo likiwa ni kuimarisha heshima ya kampuni hiyo.
Hivi karibuni SGA iliadhimisha miaka 37 tangu ilipoanza shughuli zake nchini Tanzania, ambapo imeshuhudia mafanikio makubwa. "Siri ya mafanikio yetu ni mapinduzi yanayolenga kuboresha huduma zetu sambamba na maslahi ya wafanyakazi wetu, pamoja na ushirikiano mzuri tulionao na wadau wengine likiwemo jeshi la polisi nchini; haya yametufanya kutoa huduma bora kwa wateja wetu kupita vile wanavyotarajia”, alisema.
Bw. Sambu kuwa mafanikio hayo pia yamechangiwa na uaminifu, uadilifu na juhudi kubwa walizo nazo wafanyakazi wa kampuni hiyo, ambapo alisema hupata ajira kwenye kampuni hiyo baada juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi wa kampuni hiyo wakati wa uteuzi, uajiri, mafunzo mema na motisha baada ya kupata ajira hizo.
"Ili kulinda mafanikio haya, tunaendelea kuboresha yote haya kupitia njia mbalimbali kama vile kuwekeza zaidi kwenye teknolojia ya ulinzi, maboresho ya motisha kwa wafanyakazi ambao kwa sasa ni zaidi ya 6,000”, alisema.
Bw. Sambu aliendelea kusema kuwa hivi karibuni kampuni ya ulinzi ya SGA imepata mafanikio mengi kutokana na utendaji wake kazi bora, ikiwa ni pamoja na tuzo ya juu iliyotunukiwa hivi karibuni ya teknolojia bora kwa makampuni ya ulinzi kwa usalama wa madini nchini wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Madini ya Geita.
Mkurugenzi Mkuu wa SGA Tanzania, Eric Sambu, pia alitangazwa kuwa miongoni mwa watendaji 100 bora nchini Tanzania pale alipotangazwa kama Mkurugenzi Mtendaji Bora wa Mwaka, tuzo aliytunukiwa hivi karibuni.
SGA pia ilishinda kura ya Mtoa Huduma za ulinzi aliye na vifaa bora zaidi na inayoaminika kupitia kura ya tuzo ya chaguo la wateja kwa mwaka wa 2020, ambapo upigaji kura wa tuzo hiyo kwa mwaka 2021 unaendelea.
Kampuni ya ulinzi ya SGA imeendelea kudumisha umahiri na ushindi wake katika nyanja tatu za ubora ambao ni pamoja na ubora katika usimamizi (ISO 9001:2015), ubora wa Afya na Usalama Kazini (ISO 45001:2018) na Mfumo wa Usimamizi wa Uendeshaji bora wa ulinzi (ISO 18788:2015).
Kampuni ya ulinzi ya SGA ilianza shughuli zake mwaka wa 1984, kama Group Four Security (T) Ltd. Inatoa huduma mbalimbali zinazojumuisha ulinzi wa watu na mali zao, ulinzi wa kielektroniki, huduma za kukabiliana na dharura mbaimbali, ufuatiliaji unaolenga kuhakikisha usalama, pamoja na usafirishaji wa vifurushi na fedha.
"Uwepo wa magari 284 na vituo 12 vya kikanda vilivyo na vyumba vya mawasiliano ya uhakika sambamba na wafanyikazi mahiri waliohamasishwa kusimamia yote haya, ni wazi ya kuwa tunayo miundo ya msingi itakayotuwezesha kutoa huduma za kuridhisha wateja wetu nchini kote”, alisema.
Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kawe SP Suphian Kasanga akikagua gwaride lilioandaiwa na walinzi wa kampuni ya SGA Security baada ya kufuza mafunzo ya mwezi mmoja katiaka academy ya kampuni hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kawe SP Suphian Kasanga akikagua gwaride lilioandaiwa na walinzi wa kampuni ya SGA Security baada ya kufuza mafunzo ya mwezi mmoja katiaka academy ya kampuni hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania Eric Sambu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...