Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kujipanga vyema ili kukirejesha katika hali ya kawaida Kituo cha Elimu ya Sayansi ya Baharini baada ya maeneo ya jengo lake kuungua moto.
Dk.
Mwinyi ametoa pongezi hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Rais
mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya nne, Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mhe.
Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa hatua ya uongozi wa Chuo hicho kujipanga
kwa ajili ya kukifanyia ukarabati kituo hicho mara baada ya ajali ya
moto iliyotokea tarehe 2 Oktoba mwaka huu, ili kiweze kurejea katika
hali yake ya kawaida na kutoa fursa ya kufanyika kwa shughuli za mafunzo
na utafiti ni jambo la kupongezwa na ameahidi Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itaunga mkono kikamilifu hatua hiyo.
Kwa upande wake
Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amemweleza Rais Dk. Mwinyi juu ya madhara ya
ajali ya moto iliyotokea kwenye Kituo hicho cha Elimu ya Sayansi ya
Baharini ambapo miongoni mwa maeneo yalioathirika na kuteketea kwa moto
ni maabara tatu pamoja na vifaa mbali mbali vya utafiti na hivyo
kusimamisha kabisa shughuli za mafunzo na utafiti.
Dkt Kikwete aliongeza kuwa kituo hicho ni muhimu sana hususani wakati huu ambapo Zanzibar inatekeleza sera ya Uchumi wa Buluu.
Wakati
huo huo, Dkt. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya
Ushirikiano wa Maji Duniani(Global Water Partnership) alimuarifu Mhe.
Rais Dk. Mwinyi maandalizi yanaendelea vizuri ya Kongamano kubwa la
Uwekezaji katika sekta ya Maji litakalofanyika visiwani Zanzibar katikai
ya mwezi ujao wa Disemba.
يعد لقاح سينوفارم من أول اللقاحات التي أطلقتها الصين لمقاومة فيروس كورنا covid19 المستجد، وقد أعلن الباحثون أنه يعطي فاعلية تزيد عن 80% بعد تناول الشخص جرعتين منه يفصل بينهما 4 أسابيع تقريبًا. لكن يحذر تناوله في حالة وجود إصابة حالية بفيروس كورونا.
ReplyDeleteلمزيد من التفاصيل في هذا الرابط
https://kyanteb.com/%d9%84%d9%82%d8%a7%d8%ad-%d8%b3%d9%8a%d9%86%d9%88%d9%81%d8%a7%d8%b1%d9%85/
يعد لقاح سينوفارم من أول التطعيمات التي أنتجت لمقاومة فيروس كورونا، ويعطى على جرعتين بينهما فارق 3 أسابيع أو 4 أسابيع ويعطي فاعلية تتخطى 80%
ReplyDeleteلمزيد من التفاصيل ممكن الدخول إلى الرابط من هنا
https://kyanteb.com/%d9%84%d9%82%d8%a7%d8%ad-%d8%b3%d9%8a%d9%86%d9%88%d9%81%d8%a7%d8%b1%d9%85/