Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kujipanga  vyema ili kukirejesha katika hali  ya kawaida Kituo cha Elimu ya Sayansi ya Baharini baada ya  maeneo ya jengo lake kuungua moto. 

Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza  na Rais mstaafu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mhe. Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa hatua ya uongozi wa Chuo hicho kujipanga kwa ajili ya  kukifanyia ukarabati kituo hicho mara baada ya ajali ya moto iliyotokea tarehe 2 Oktoba mwaka huu, ili kiweze kurejea katika hali yake ya kawaida na kutoa fursa ya kufanyika kwa shughuli za mafunzo na utafiti ni jambo la kupongezwa na ameahidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaunga mkono kikamilifu hatua hiyo.

Kwa upande wake Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete  amemweleza Rais Dk. Mwinyi juu ya madhara ya ajali ya moto iliyotokea kwenye Kituo hicho cha Elimu ya Sayansi ya Baharini ambapo miongoni mwa maeneo yalioathirika na kuteketea kwa moto ni maabara tatu pamoja na vifaa mbali mbali vya utafiti na hivyo kusimamisha kabisa shughuli za mafunzo na utafiti.

Dkt Kikwete aliongeza kuwa kituo hicho ni muhimu sana hususani wakati huu ambapo Zanzibar inatekeleza sera ya Uchumi wa Buluu.

Wakati huo huo, Dkt. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushirikiano wa Maji Duniani(Global Water Partnership) alimuarifu Mhe. Rais Dk. Mwinyi maandalizi yanaendelea vizuri ya Kongamano kubwa la Uwekezaji katika sekta ya Maji litakalofanyika visiwani Zanzibar katikai ya mwezi ujao wa Disemba
.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. يعد لقاح سينوفارم من أول اللقاحات التي أطلقتها الصين لمقاومة فيروس كورنا covid19 المستجد، وقد أعلن الباحثون أنه يعطي فاعلية تزيد عن 80% بعد تناول الشخص جرعتين منه يفصل بينهما 4 أسابيع تقريبًا. لكن يحذر تناوله في حالة وجود إصابة حالية بفيروس كورونا.
    لمزيد من التفاصيل في هذا الرابط
    https://kyanteb.com/%d9%84%d9%82%d8%a7%d8%ad-%d8%b3%d9%8a%d9%86%d9%88%d9%81%d8%a7%d8%b1%d9%85/

    ReplyDelete
  2. يعد لقاح سينوفارم من أول التطعيمات التي أنتجت لمقاومة فيروس كورونا، ويعطى على جرعتين بينهما فارق 3 أسابيع أو 4 أسابيع ويعطي فاعلية تتخطى 80%
    لمزيد من التفاصيل ممكن الدخول إلى الرابط من هنا
    https://kyanteb.com/%d9%84%d9%82%d8%a7%d8%ad-%d8%b3%d9%8a%d9%86%d9%88%d9%81%d8%a7%d8%b1%d9%85/

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...