Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Nicolaus Herman Shombe kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Kabla ya uteuzi huo Dkt.
Shombe alikuwa Kamishna wa Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt. Shombe anachukua
nafasi ya marehemu Prof. Damian Gambagambi ambaye alifariki akiwa katika nafasi
hiyo.
Uteuzi huo umeanza tarehe
29 Oktoba, 2021.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...