Na.Vero Ignatus,Dar es Salam.


Waandishi wa Habari za Mitandao Tanzania wametakiwa kuwa makini kwa kuandika Habari zenye takwimu sahihi, zenye uthibitisho,pamoja na kuacha kuandika vichwa vya habari visivyo na uhalisia, kwa lengo la kuwavutia wasomaji /watazamaji,huku wakitambua kuwa ni upotoshaji

Nuzulack Dause ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Nukta Africa, amesema kwa sasa Waandishi wengi ,wanaandika Habari zisizo na vigezo, huku wakiacha masuala mengi yenye ukweli,hivyo amewaasakuangalia mambo muhimu ya kuzingatia katika kutumia habari, nikujiridhisha kwa kuangalia chanzo cha habari hiyo husika.

Alieleza kuwa, kumekuwa na baadhi ya watu ama taasisi kufungua ‘account’ za mitandao kwa ajili ya kuandika na kurusha taarifa zisizo sahihi, hivyo mhariri akizitumia taarifa hizo kama zilivyo bila ya kutumia njia za kutafuta usahihi watajiingiza kwenye makosa.

Ameongeza kuwa changamoto kubwa inayosababisha hali hiyo, ni baadhi ya wamiliki wa Vyombo vya Habari mitandaoni kujali idadi ya watu wanaotembelea mitandao yao.bila kuangalia kama habari walizoweka zinasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Awali akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMF, Dastan Kamanzi alisema Waandishi wa Habari wanatakiwa kuwa na msingi wa awali, jumla na wa kubobea katika uandikaji wa habari.

Kamanzi :msingi wa uandishi wa Habari ni ukweli hivyo ni vyema kuzingatia kila wanapoandaa habari zao ni kuepuka ujanja na uongo,pamoja na kuamua kuwa wabobezi katika eneo fulani litakalokuwa linamtambulisha

''Tafuteni changamoto za jamii na kuzitafutia suluhisho na siyo kuandika habari ambazo hazina uhakika ,mnawachosha wasomaji wenu''alisema Kamanzi

Kwa upande wake msiriki wa mafunzo hayo Wilium Bundala kutoka Radio Kahama alisema mafunzo hayo yatamsaidia kuboresha uandishi wake wa habari hususani kutumia takwimu na kuhakiki habari kabla ya kuchapishwa mtandaoni.

Bundala alieleza kuna mitandao mbali mbali duniani inaweza kutumika kwa ajili ya kutuma habari za uzushi, kama vile Twiter, facebook, hivyo lazima kuwe na uchunguzi ambao utamridhisha mtumiaji wa habari hizo kabla ya kuchapisha habari husika

Aidha Mafunzo hayo ya siku tano ya Uhakiki wa Habari,yanayoendelea Jijini Dar es salaam, yamejumuisha Waandishi wa Habari za mtandaoni kutoka mikoa ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mara, Mbeya na Iringa.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo siku tano yaliyoandaliwa na TMF Jijini Dar es Salaam juu ya Uthibitishaji wa habari (Fact Checking) leo tarehe 1 novemba 2021
Mkurugenzi mtendaji wa Nukta Africa Nuzulack Dausen Akiwa anaonyesha umuhimu wa kutumia Data sahihi katika uandishi wenye tija

Mkurugenzi mtendaji wa Tanzania Media Foundation (TMF) Dastan Kamanzi akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 1 novemba2021 Jijini Dar es saam
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari kupitia vyombo vya habari mtandaoni wakifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya mtandaoni wakifuatilia mafunzo kuhusu uhakiki wa taarifa (fact cheking) yanayotolewa na TMF.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa makini ukumbini.
Mmoja wa washiriki akifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya mtandaoni wakifuatilia mafunzo kuhusu uhakiki wa taarifa yanayofanyika jijini Dar es salaam.


Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo..
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya Habari vya Mtandaoni wakifuatilia mafunzo ya uhakiki wa taarifa yaliyoandaliwa na TMF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...