Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Maulid Walad Mwatawala
kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Prof. Mwatawala anachukua
nafasi ya Prof. Bernadeth Killian ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi huo umeanza tarehe 30
Oktoba, 2021.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...