Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 11 Novemba, 2021 ameendelea na Ziara yake ya Kiserikali katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa kutembelea mji mpya wa Serikali wa Cairo (New Cairo Administrative City).

Serikali ya Misri ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha kuhamisha Makao Makuu ya Serikali katika mji mpya. Katika mji huo mpya inatarajiwa Wizara, Taasisi za Serikali, Bunge, Mahakama, Balozi za nje zenye uwakilishi nchini Misri ikiwemo Tanzania na nyinginezo kuhamia kwenye eneo hilo ambalo pia litakapokamilika linatarajiwa kuwa na watu takribani milioni 6.5.

Aidha, Mhe. Rais Samia ametembelea eneo la viwanda la Kampuni ya Elsewedy ambao ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa nchini Misri wanaokusudia kujenga eneo la uwekezaji viwanda nchini Tanzania.

Kampuni ya Elsewedy pia ndio mkandarasi mkuu wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere kwenye mto Rufiji. 

Mhe. Rais Samia pia ametembelea Taasisi ya uwekezaji na biashara huria (General Authority for Investment and Free Zones) ambayo ni Mamlaka Maalum iliyo chini ya Wizara ya Uwekezaji yenye dhamana ya biashara na kutoa motisha maalum kwa wawekezaji kwenye maeneo husika na pia utoaji vibali vya biashara na uwekezaji nchini Misri.

Katika Taasisi hiyo, Mhe. Rais Samia amekutana na Wawekezaji mbalimbali na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wawekezaji hao wa Misri kuja Tanzania kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo, madini, nishati ya umeme, elimu na nyinginezo.

Mhe. Rais Samia ameshuhudia utiaji sani wa hati za Makubaliano kati ya Tanzania na Misri katika kukuza uwekezaji kwa nchi hizo mbili.

Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa mji mpya wa kiserikali wa New Cairo Administrative City unaoendelea kujengwa Jijini Cairo nchini Misri, alipotembeleleo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mji huo leo tarehe 11 Novemba 2021. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia ramani ya mji mpya wa kiserikali wa New Cairo Administrative City unaoendelea kujengwa Jijini Cairo nchini Misri, alipotembeleleo katika Makumbusho mapya yaliopo katika mji mpya wa Kiserikali Cairo Misri leo tarehe 11 Novemba 2021. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji saini Hati za makubaliano katika Nyanja ya kukuza Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Biashara Huria nchini Misri Dkt. Mohammed Abdul-Wahabi leo tarehe 11 Novemba 2021 Jijini Cairo Misri. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia mabadilishano ya Hati za makubaliano katika Nyanja ya kukuza Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Biashara Huria nchini Misri Dkt. Mohammed Abdul-Wahabi leo tarehe 11 Novemba 2021 Jijini Cairo Misri. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa Misri baada ya kuzungumza na Wafanyabiashara hao leo tarehe 11 Novemba 2021Jijini Cairo nchini Misri, ambapo amewaelezea fursa mbalimbali za uwekezaji ziliopo nchini Tanzania. Mhe. Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mji mpya wa New Cairo Administrative City Jijini Cairo nchini Misri leo tarehe 11 Novemba 2021. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea na ziara ya Kiserikali ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mji mpya wa New Cairo Administrative City Jijini Cairo nchini Misri leo tarehe 11 Novemba 2021. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea na ziara ya Kiserikali ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...