Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

WARAIBU wa dawa za kulevya walioko katika nyumba ya matibabu (Sober House) ya Free at Last Kihonda mkoani  Morogoro wametoa ombi kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kuwasaidia katika kuwalipia pango la nyuma na chakula ili kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma ya kuwasaidia vijana walioamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Wametoa ombi hilo leo Novemba 11,2021 baada ya kutembelewa na maofisa wa Mamlaka hiyo walioambatana na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari 30 waliofika katika nyumba hiyo kwa lengo la kujifunza na kuona maisha halisi wanayoshi vijana wenye uraibu wa dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Kituo cha Upataji nafuu cha Free at Last Sober House Michael Kassian amesema wamefurahi kuona wametembelewa na maofisa wa  Mamlaka hiyo pamoja na waandishi wa habari kwani itafungua milango ya wao kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

"Tumekuwa tukiwasaidia vijana wenzetu katika kuwapatia matibabu kwa zaidi ya miaka sita na mkapa sasa tumesaidia vijana zaidi ya 620 na programu zetu zimejikita katika mabadiliko ya tabia kwa vijana wanaotumia dawa za kulevya , tunawaita waraibu.Katika kituo hiki tunao waraibu 11 

"Tunashukuru kwa ushirikiano ambao tunaupata kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya,wamekuwa wakitoa kila aina ya ushirikiano kwetu.Tunafaraha kuwaona waandishi wa habari ambao wamefikiria kuja kwetu na tunaamini kama tutashirikiana na vyombo vya habari tutafika mbali,"amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu kituo chao amesema wanachangamoto nyingi lakini kama Waraibu wana changamoto nyingi huku akisisitiza dawa za kulevya ni changamoto na ni janga kubwa katika jamii, hivyo elimu inahitajika na hapo mchango wa waandishi wa habari unahitajika.

"Changamoto za kituo tunasaidia vijana ambao wamechokwa na familia ,wamechokwa na jamii kwa hiyo wanavyokuja hapa wanakuja mmoja mmoja wakiwa hawana msaada wowote.Hatuna wadhamini kwa hiyo kupitia ujio wenu tunaweza kupata wadhamini ili tulipe kodi ya pango na kununua chakula.

"Tuna watu ambao wanajitoa katika masomo maana nao walipitia katika utumiaji dawa za kulevya, hivyo wanajitolea kusaidia wengine, hivyo tukipata chakula na kodi ya jengo tutafika mbali zaidi.Tukifanikiwa katika hayo mawili basi tutajikita zaidi kuwasaidia waraibu walioko  hapa,"amesema.

Ameongeza Waraibu wengi mfumo wao wa maisha umeharibika , na ukiangalia kwa haraka unaweza kuoa watu hao walitaka , unaweza kuona hilo ni tatizo ni la Mraibu peke yake, lakini hilo ni janga la jamii."Kuna wazazi wamefariki kwa presha kwasababu ya watoto kutumia dawa za kulevya. Ni tatizo kwa Serikali kwani tunaona inavyotumia gharama kubwa kuwatibu waraibu."

Kwa upande wake Abel Leonard ambaye ni mmoja ya vijana walioko kwenye kituo hicho cha matibabu amesema yeye sio mara ya kwanza kukaa kwenye kituo cha matibabu, alishakaa huko nyuma na sasa amerudi tena baada ya kuona hali imekuwa mbaya.

"Nilijiingiza kwenye dawa za kulevya ili kukimbia uhalisia, na sababu kubwa ilitokana na kuondokewa na wazazi wake, kabla ya kutumia dawa za kulevya aina ya heron alikuwa anakunywa pombe na kuvuta bangi, hivyo nikajikuta anaingia katika utumiaji wa dawa kwa ajili ya kutafuta furaha niliyokuwa naikosa.

"Baada ya kupitia changamoto, sikupata washauri wazuri, naamini ningeshauriwa vizuri nisingejiingiza kwenye kutumia dawa za kulevya.Ushauri wangu hata ukikutana na changamoto simama katika njia sahihi kukabiliana nayo na si kikumbilia kutumia dawa za kulevya,"amesema.

Awali Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DCEA Florance Khambi amesema sababu waandishi kutembelea kituo hicho ni kujifunza namna ambavyo waraibu walioko katika kituo hicho wanavyoishi na jinsi ambavyo wanaendelea kupata matibabu na ujumbe mkubwa ni kuiambia jamii ya Watanzania kuwa dawa za kulevya ni tatizo ambalo linatibika na matibabu yake yapo."Tumekuja hapa tukiwa kwenye ziara ya mafunzo , tuko na wanahabari za kidigitali, kwa hiyo tumefika hapa kwenye nyumba ya utengamao ya Sobae House Free at last kujifunza".

Kikapu kikiwa na fedha ambazo zimechangwa na waandishi wa habari za digitali baada ya kutembelea kituo cha upataji nafuu cha Free at Last Sober House kilichopo Kihonda mkoani Morogoro.Fedha hizo ni kwa ajili ya kuwachangia waraibu wa dawa za kulevya wanaopata matibabu katika kituo hicho.

Mkurugenzi wa Kituo cha upataji nafuu cha Free at Last Sober House Michael Kassim akizungumzia programu wanazofanya kituoni hapo katika kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya

Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi akielezea aina ya matibabu yanayotolewa kwa waraibu wa dawa za kulevya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...