· Washindi watatu wajinyakulia vifaa vya DJ zenye thamani ya milioni saba TSH kila mmoja.
Arusha.
Bia pendwa ya Serengeti Lite imehitimisha shindano lake la DJs
lililopewa jina la Take a Bite Out of Life kwa kuwatunuku ma-DJ watatu
bora nchini vifaa vya kupigia mziki zenye thamani ya shilingi million
saba kila mmoja kwenye ukumbi wa Triple-A ambapo ilishindanisha
washiriki saba wa mwisho kutoka kanda tofauti nchini.
Tukio
hili lilihitimisha kampeni ya miezi mitatu kwa kupata ma-DJ watatu
kutoka kanda saba nchini. Pia washindi hawa wamepata fursa adimu za kuwa
ma-DJ rasmi wa chapa ya Serengeti Lite katika promosheni na shughuli
zake za utangazaji nchini.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha
hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bia cha SBL, Nandy Mwiyombella, alisema,
'Ni wakati wa kusisimua kwa SBL na bia yake ya kipekee, Serengeti Lite,
ambayo imetumia shindano hili ili kuwasaidia vijana kuonyesha vipaji
vyao. Serengeti Lite ina shauku ya kuwaona vijana kuonyesha umahiri wao
katika vipaji walivyonavyo’.
Aliendelea, ‘Vilevile shabaha ya
Take a Bite out of Life ililenga kutoa burudani kwa wateja wetu katika
maeneo waliyopo ili waendelee kufurahia kinwyaji chenye ladha kamili cha
Serengeti Lite, Bia ya Kitanzania iliyotengenezwa kwa ajili ya
Watanzania na ya Watanzania’.
Afisa Vijana wa Arusha Japhet
Kurwa ndiye aliyeongoza hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. John
Mongella ambaye pia aliwatunuku washindi watatu waliobahatika. Kurwa
alipongeza juhudi za SBL za kuchochea soko la ajira kwa kutoa motisha
kwa vijana katika sekta ya burudani.
Kurwa alisema, ‘nimejawa
na furaha kubwa sana baada ya kushuhudia jinsi vijana wanavyopambania
ndoto zao kwa nguvu na ari. Nawapongeza sana SBL kwa kutimiza ndoto zao.
Ni siku nzuri kwa washindi hawa watatu; maisha yao hayatakuwa sawa tena
kwa sababu fursa hii imekuwa chanzo cha ajira kwao. Nina uhakika pia
kuwa washiriki wengine (hasa washindi) mtaanza kupokea mialiko mingi
kwenye hafla za kutumbuiza mziki maeneo mbalimbali na pengine kufungua
studio zenu za muziki hapo baadae.
Kurwa aliendelea kusema,
‘tukio la leo limekuwa gumzo na kuibua hisia nzuri sana kwa vijana hapa
mjini Arusha. Ni matumaini yetu kama Serikali ya mkoa kuwa vijana
wamehamasika kujiinua kimaisha na kuchangamkia kila fursa zingine
zilizopo ili kufikia malengo yao hasa katika hiki kipindi ambacho
Serikali yetu inafanya kazi kubwa ya kuongeza ajira nchini’.
Kampeni
ya Take a Bite Out of Life iliambatana na shughuli za burudani kutoka
ma-DJs wa ndani walioshindana katika wilaya na mikoa nchini kote.
Shindano hili lilishirikisha zaidi ya washindani 5,200 wenye zaidi ya
miaka 18 wenye matarajio ya kujenga vipaji vyao kama waburudishaji wa
muziki.
Katika kila tukio, washiriki waliobahatika waliondoka
na zawadi mbalimbali na zaidi ya hayo jukwaa hili liliwapa fursa ya
kuonyesha vipaji vyao mbele ya majaji maarufu kama vile DJ ZERO na umma
kwa ujumla.
Hii si mara ya kwanza kwa SBL kuwekeza katika miradi
kama hii. SBL pia imewekeza katika sekta ya michezo kwa kudhamini timu
ya Taifa Stars, ligi ya Taifa ya Wanawake na mashindano mengine muhimu
ya gofu.
Mkuu wa Kitengo cha Bia wa Kampuni ya Serengeti (SBL), Nandy Mwiyombella (kulia) na Katibu wa chama cha MaDJ nchini, Asanterabi Mtaki (kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza wa shindano la DJ compee, Take a Bite Out of Life, Abdulaziz Juma maarufu Dj Dully Tz kutoka Dodoma, ambaye pia alipata seti ya vyombo vya muziki wa uDJ vyenye thamani ya shilingi milioni 7 kutoka kampuni ya SBL. Shindano hilo lililowashirikisha wachezesha muziki zaidi ya 5,200 kote nchini na fainali zake zilifanyika jijini Arusha usiku kuamkia jumapili.
Mkuu wa Kitengo cha Bia wa Kampuni ya Serengeti (SBL), Nandy Mwiyombella akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa shindano la DJ compee, Take a Bite Out of Life, Mussa Shaban maarufu Dj. Son kutoka mkoa wa Kilimanjaro shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti Tanzania SBL lenye lengo la kuwasaidia vijana kuweza kujiajiri.
Afisa anayeshughulika na masuala ya vijana wa Mkoa wa Arusha, Japhet Kurwa (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Basata, Matiko Mniko (kushoto) na Afisa Sanaa wa Basata, Joseph Mmbigo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...