Na Mwandishi wetu, Mbeya
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali itatenda haki katika mchakato wa kuwapata washindi wa tuzo za filamu kwa mwaka 2021.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Mbeya wakati akielezea maandalizi ya kilele cha Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2021.

“Kwa kuzingatia ukweli kwamba hizi ni Tuzo za kwanza za Serikali, hivyo Serikali haitakuwa sehemu ya kumnyima mtu haki ya ushindi kama kweli anastahili kushinda pasipo kutazama jina au umaarufu wa mtu, hata Wasanii wachanga wana haki ya kushinda Tuzo hizi”. Alisema Mhe. Bashungwa.

Waziri Bashungwa alieleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan imeanzisha Tuzo hizo kwa mara ya kwanza kwa lengo la kutambua mchango wa Wanatasnia ya Filamu nchini ambapo kilele kitafanyika Desemaba18, 2021jijini Mbeya katika ukumbi wa Tughimbe.

Akielezea sababu ya kilele cha Tuzo hizo kufanyika jijini Mbeya amesama ni kutambua uwepo wa Wanatasnia ya Filamu pamoja na Wasanii wengine kwa ujumla wake Jijini humo, pamoja na kufungua milango ya fursa mbalimbali zilizoko Mbeya ikiwemo kutumia Tuzo hizo kuonesha vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyopatikana jijini humo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema kupitia tuzo hizo ni fursa ya kipekee kwa wadau wa maendeleo kutembelea Mkoa wa Mbeya kujionea uzuri wake na kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...