Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
SERIKALI
imejipanga kuhakikisha inaokoa takribani nusu trilioni ya fedha ambazo zimekuwa
zikienda nje kila mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kupikia kwa kuja na
mbegu za kisasa, kuboresha shughuli za ugani pamoja na tafiti ili
kujitosheleza.
Akifungua kongamano linalojadili sera za namna Tanzania inavyoweza kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia mkoani Dar es Salaam jana, Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda alisema kiasi hicho kikiokolewa, kitasaidia katika kuchangia uchumi wa ndani na kutengeneza ajira zaidi kwa vijana.
"Tunazalisha
wastani wa asilimia 45 tu ya mahitaji yetu na tunatumia wastani wa Sh bil 475
kila mwaka, karibu nusu trilioni. Unapopeleka kiasi hicho nje, unaenda pia
kuboresha ajira nje. Kwa miaka mitatu tunakuwa tumepeleka nje zaidi ya fedha
tulizokopa hivi karibuni IMF, Sh trilioni 1.3.
"Angalia hizo fedha za IMF zinavyofanya kazi nyingi kwa hiyo zikibaki ndani zitapunguza tatizo la ajira. Machinga wengi watakuwa wanazalisha viwanda badala ya kuwa baranarani," alisema.
Akizungumzia
kuhusu hatua zinazochukuliwa alisema ni pamoja na kusambaza mbegu bora za mazao
yanayozalisha mafuta kwa wingi kama chikichi, alizeti, ufuta, karanga na
nazi.
Kwa
upande wa alizeti ambayo kwa sasa inaongoza kwa kuzalisha mafuta kwa wingi
nchini alisema kwa sasa mkulima anapata wastani wa tani 0.7 kwa ekari wakati
akitumia mbegu bora na kilimo cha kisasa anaweza kupata hadi tani 4.0 kwa
ekari.
Kingine
ambacho serikali imedhamiria kufanya alisema ni kuongeza bajeti ya shughuli za
ugani na utafiti.
Kwa
upande wa maofisa ugani alisema serikali itanunua pikipiki 2,000 ambazo
zitagawiwa kwa maofisa ugani hivi karibuni, pamoja na kuwa na vifaa vya kupimia
udongo na simu janja.
Waziri
alisema mpaka sasa Tanzania ndio inaongoza kwa kuzalisha mafuta ya kula Afrika
Mashariki na ni ya 26 duniani, Ukraine ikiongoza.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wazalisha Mafuta ya Kupikia (TASUPA), Ringo Iringo, alisema
kutokana na uzalishaji mdogo, viwanda vingi vinafanya kazi kwa kipindi cha
miezi mitatu hadi minne na Kufunga kwa kukosa malighafi.
Alisema
Tanzania ina viwanda takribani 775 kuanzia vidogo kabisa hadi vikubwa.
Alishauri
mashamba yaongezwe akisema kwani mafuta ya kupikia ni ya lazima nyumbani kuliko
hata Mazao kama korosho.
Naye
Mratibu wa Kitaifa wa Mazao ya Mafuta ya Kupikia kutoka Taasi ya Utafiti wa
Kilimo Tanzania (Tari), Joseph Nzunda alisema kimsingi Tanzania ina ardhi ya
kutosha kuzalisha mafuta ya kula hadi kuuza nje, akisema soko ni kubwa sana.
Alisema mbegu bora kwa sasa zipo zonazoweza kuleta tija maradufu kwenye uzalishaji kinachotakiwa ni mipango bora.
Kongamano hilo limeandaliwa na
wizara ya fedha na Mipango kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya-EU.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...