Rais wa Zannzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-Haji Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa Dini ya Kislamu kutumia maadhimisho ya Mazazi ya Mtume Muhamad (S.A.W) kwa kudumisha Amani na mshikamano katika jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo wakati akimuwakilisha Rais Dk. Mwinyi katika sherehe za Maulid ya Kusifu Mtume S.A.W yalioandaliwa na waumini wa Tumbatu Jongowe Mkoa wa Kasakazini Unguja.
Alisema kuwa, moja kati ya Sifa za Mtume Muhamad S.A.W alikuwa ni kiongozi mwenye sifa ya kuwaunganisha na kuwaleta pamoja watu kwa kutumia maelekezo ya Dini ya kislamu bila ya kujali tofauti zao.
Mhe. Alifafanua kuwa kuna kila sababu kwa waumini na wananchi wa Tumbatu Jongoe na maeneo mengine kuiga kigezo chema kutoka kwa kiongozi wa Umaa wa Kisalamu kwa kudumisha Umoja, upendo na mshikamano bila ya kujali tofauti zozote walizonazo ikiwemo tofauti za kisiasa.
Aidha, aliwahakikishia wananchi wa Tumbatu Kuwa, serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi itahakikisha shughuli za wananchi zinaendelea vyema kwa kuwafikishia huduma za msingi ikiwemo masuala ya kimaendeleo.
Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais aliwakumbusha waumini hao kuendelea kumuombea Dua Rais Dk. Mwinyi ili Mwenyezi Mungu amewezesha kuyatekeleza yale yote aliyoyaahidi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Kabla ya Kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu Mufti Mkuu Sheikh Mahamoud Mussa Wadi aliwakumbusha waumini hao kushikamana na muongozo wa Dini ya kisalamu unaowataka waislamu kuishi pamoja na kuachana na tofauti ili kupata radhi za Allah (S.W).
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahamoud aliwataka wananchi wa Tumbatu na Zanzibar kwa Ujumla kuzitumia sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume (S.A.W) kwa kuwaunganisha wananchi wote kuwa kitu kimoja.
Mamia ya waumini kutoka Tumbatu Jongowe walishirikiana pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika sherehe ya Maulid ya Mtume Muhamad (S.A.W) yaliofanyika kijijini humo.
:Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipokea zawadi maalum kwa niaba ya Rais Dk. Mwinyi iliyoandaliwa na Waumini na wananchi wa Tumbatu Jongowe.
Wanafunzi wa madrasa mbali mbali za Tumbatu Jongowe wa wakisherehesha kwa kucheza Kasida kwa ustadi mbele ya Mgeni rasmi katika sherehe za Maulid ya kumsifu Mtume (S.A.W).
Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleima Abdulla akizungumza na waumini wa Dini ya Kislamu katika sherehe za mazazi ya Mtume Muhamad (S.A.W) zilizofanyika Tumbatu Jongowe ambapo Mhe. Hemed amemuwakilisha Rais Dk. Mwinyi.
Waumini mbali mbali kutoka viunga vya Tumbatu Jongowe wakifuatilia Nasaha za Mgeni rasmi Mhe. Hemed alizozitoa katika Sherehe za Maulid ya kumsifu Mtume (S.A.W) ambapo aliwahimiza waumini hao hao kushikamana pamoja katika Dini ya Allah (S.W)
Mhe. Hemed akiwasalimia wananchi wa Tumbatu Jongowe wakati akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya kushiriki katika Sherehe za Maulid ya kumsifu Mtume (S.A.W).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...