Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imefanikiwa kutoa mikopo yenye jumla ya thamani ya zaidi shilingi bilioni 391 kwa ajili ya kuendeleza Kilimo na imeaahidi kuendelea kutoa mikopo zaidi.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa TADB Frank Nyabundege alisema lengo la benki hiyo ni kuwafikia wakulima wengi zaidi
Mkurugenzi huyo alisema ili kuwafikia wakulima wengi zaidi,benki hiyo imekuwa ikichagiza mabenki ya biashara kukupesha wakulima kupitia dhamana ambazo benki hiyo imekuwa ikitoa kwa mabenki mbali ya biashara ya mtandao mpana nchi nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege(kushoto) akipata maelezo juu ya shughuli za kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Tanga Fresh kutoka kwa maofisa wa kiwanda hicho ambao walishiriki katika maonyesha ya wiki ya huduma za kifedha jijini Dar es Salaam. Kiwanda cha Tanga Fresh ni moja kati ya wanufaika wa mikopo inayotolewa na benki ya kilimo
Meneja wa Mfuko wa Dhamana kwa wateja wadogo wa Benki ya Kilimo (TADB), Asha Tarimo (kushoto), akimuelekeza faida ya kutumia benki hiyo mteja aliyetembelea banda la benki hiyo, Yahaya Duru, katika maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.
Wateja waliotembelea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakipata maelezo ya shughuli mbali mbali ambazo zinafanywa na baadhi ya wanufaika wa mikopo inayotolewa na benki hiyo katika maonyesho ya huduma za kifedha yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...