Na Khadija Seif, Michuzi TV
KAMPUNI ya Chocolate Princess imetangaza atangaza usiku wa Tamasha la Vyakale Dhahabu utakaofanyika Desemba 10 mwaka huu Mlimani City mkoani Dar es salaam ambapo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Akizungumza leo Novemba 8,2021, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mboni Masimba amesema usiku huo wa tamasha la Vyakaleya Dhahabu pamoja na mambo mengin utakuwa sehemu ya kusherehekea miaka 60 ya uhuru wa nchi ya Tanzania.
"Tunaposherehekea miaka 60 ya Uhuru wa nchi yetu pia tutaitumia kusherehekea pia Wakongwe wetu kwenye tasnia hii ya muziki wa taarabu,hivyo kwa mara hii tumeandaa tamasha hili kwa ajili ya kukonga nyonyo za wapenzi wa muziki wa mwabao hasa waimbaji taarab wakongwe," amesema.
Masimba amewataja watakaosindikiza usiku huo wa burudani ya aina yake akiwemo Sabaha Muchacho,Khadija Kopa,Abdul Misambano,Afua Suleiman, Patricia Hillary na wengine wengi.
Ameongeza kusiku huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwetehuku akikitaja kingilio hicho wazi kuwa ni elfu 50 za Kitanzania ikijumuishwa chakula na vinywaji.
Moja ya wadhamini katika tamasha hilo kutoka Kampuni ya ulinzi K4 Security Biko scanda amesema wanayofuraha kuwa sehemu ya Tamasha la vya Kale dhahabu na kuhakikisha Kuna usalama wa raia na Mali zao.
"Sisi ni sehemu ya kila historia nzuri nchini,sisi ni wakali wa Kazi zote za ulinzi na hakika tunaifanya Tanzania kujivunia Kampuni yetu."
Mkongwe wa taarab ambaye pia ni Mama Mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa amempongeza Mboni kwa kuandaa Tamasha Hilo lenye Lengo la kuwaburudisha wapenzi wa Mwambao.
"Mtoto wetu ameandaa Tamasha ambalo linatoa Burudani kwa Mashabiki zetu pia tunapata wasahaa wa kuwaenzi waliotangua kama Leila Khatib,Omary Kopa."
Mkongwe wa Taarab nchini Afua Suleiman akitoa pongezi kwa Muandaaji wa Tamasha Hilo Mboni Masimba kwa kuandaa Tamasha Hilo lenye Lengo la kuwapa Burudani wapenzi wa Taarab
Meneja Masoko Kampuni ya ulinzi Ks4 Security Biko Scanda akiwatoa hofu wapenzi wa Taarab kuwa usalama utaimarika kwa kiwango Cha juu kupitia Kampuni yao katika "Tamasha la vya Kale dhahabu"
Muimbaji wa Taarab nchini Khadija Kopa akizungumza kuhusu Tamasha "la vya Kale dhahabu" akiwataka wapenzi wa Muziki wa Taarab kujitokeza kwa wingi huku wakivalia Mavazi ya heshima
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...