Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme,akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi pamoja na watumishi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) ambao walifanya ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar,akielezea jambo wakati wa ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) akimsikiliza Mhandisi ujenzi katika eneo la Viwanda vya Tofali na Zege Athu Chulla akitoa maelezo ya mradi katika eneo la Nzuguni wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi akiangalia ujenzi wa mradi katika Mji wa Kiserikali Mtumba wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua,kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme,akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi kwa kutembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar,akielezea jinsi walivyojifunza katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
.............................................................
Na.Mwandishi Wetu,Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi amesema mpango uliopo kwa sasa ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kushirikiana na Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) katika kutekeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 26,2021 wakati wa ziara ya Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Miradi hiyo ni pamoja na ule wa Mji wa Kiserikali Mtumba awamu ya pili,mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 wa watumishi wa umma,Nzuguni ambao umeanza na nyumba 150 na mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi katika eneo la Kisasa.
Katibu Mkuu Kilangi amesema kwa sasa wanaiamini TBA kwa asilimia mia moja hivyo watashirikiana na ZBA kutekeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar kwa lengo la kupata miradi yenye ubora kama Tanzania Bara.
“Sasa mimi nadhani tuiamini TBA kwa asilimia miamoja kama tunamiradi tutakayoianzisha basi TBA na wana miradi Zanzibar tutawaleta wataalamu wetu waje wafanye kazi kwa pamoja na TBA.
“Wanzanzibar wategemee tutawaalika TBA Zanzibar, wategemee mambo mazuri hizi fedha tulizopata tuna bilioni 460 zinaenda mifukoni mwa watu kupitia miradi mbalimbali.Tutawambia waje Zazibar wasimamie miradi yetu,”amesema.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza yale ambayo TBA wanayafanya ambapo kwa kiwango kikubwa yanalingana na majukumu ya ZBA.
''Zanzibar kwa sasa wapo katika matayarisho ya Mji wa Kiserikali visiwani humo ambapo utekelezaji wao utakuwa ni mkubwa ambapo amewakaribisha TBA waone yale ambayo wameyaonesha tutakavyoyatekeleza.''amesema Mhandisi Omar
Naye,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme amesema ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwani ZBA wameweza kuona mradi wa nyumba za watumishi wa umma na wameona jinsi walivyoutekeleza mradi huo na wameweza kujionea jinsi ambavyo wamejipanga katika eneo la material pamoja na viwanda mbalimbali ambavyo wamevianzisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya ujenzi TBA,Likimaitare Naunga ameishukuru ZBA kwa kuichagua TBA kama sehemu ya kupata uzoefu katika sekta ya ujenzi ambapo amedai wapo tayari kwa ajili ya ushirikiano huo.











Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...