Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Francis Nanai akizungumza katika uzinduzi wa mradi Africa Franchising Accelerator wa kukuza chapa za wafanyabiashara kuwa wakubwa kwa chapa hizo kuwa ulimwenguni kote katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hotel ya Four Points zamani New Afrika.
Mkurugenzi wa Miradi TPSF Julius Wambura akizungumza kuhusiana na mradi wa AfRAP wa kunuinua biashara za wafanyabiashara wadogo katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Franchiese, Damas Mugashe akitoa kuhusiana na wanachama kuchangamkia fursa za mradi wa AfRAP katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza akizungumza kuhusiana na fursa hiyo kwa wanawake wafanyabiashara kuchangamkia katika uzinduzi mradi wa AfRAP jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa mradi AfRAP Wambugu WA Gichohi akizungumza namna mradi utapotekelezwa na kuleta tija kwa Taifa,Jijini Dar es Salaam.
*Rais Samia Suluhu Hassan amefungua milango ya uchumi.Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imepata msaada wa zaidi ya Milioni 700 kwa ajili ya kuendeleza wafanyabiashara wadogo kukua na chapa zao na kuuza duniani kote.
Msaada huo ni kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ambapo Tanzania kwa nchi za Afrika Mashariki ndio ya kwanza kuwa na Mradi huo unaojulikana kama Africa Franchising Accelerator (AFRAP) 2021-2025.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Francis Nanai amesema mradi utazalisha ajira za moja kwa moja 38,000 na zile zisizo moja kwa moja ni ajira 56,000.
Amesema kuwa wafanyabiashara wa wakikuza chapa na kuuza duniani kote watasaidia katika ukuaji wa uchumi na kufanya nchi kuwa imara kiuchumi.
Nanai amesema kuwa baadhi ya kampuni ambazo zilianza ukuaji huo ni Pepsi, Coca Cola, KFC ambazo Chapa zake zilikuwa zinauzwa na kueneaa Duniani hali ambayo wafanyabiashara wadogo wanaanza kujengwa kufika huko.
Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefungua Uchumi wa Nchi hivyo ni kazi ya watanzania kuchangamkia fursa hiyo ambapo TPSF ipo kwa ajili ya kuona biashara zinakua kwa kasi.
Nanai amesema kuwa vigezo vya kuingia kwa wafanyabiashara wadogo kwanza ni kuwa na leseni za biashara ,kampuni zao ziwe zimekaguliwa mahesabu kwa miaka mitatu mfululizo,Mauzo ya Biashara kwa mwaka sh.milioni 250 pamoja na ulipaji kodi katika mifumo iliyowekwa na nchi.
Amesema mradi utachukua miezi 48 ambapo wataanza na mafunzo visiwani Zanzibar kuanzia November 22 mwaka huu na kwenda Jijini Mwanza ,Mbeya na Mikoa mingine huku Dar es Salaam kupata mafunzo 2022.
"Mradi huu haufanywi kihuni huni ndio maana vigiezo hivyo ni kwa ajili ya kupata washindani ambao wanauwezo wa kukuza chapa zao na Taifa kuwa na wafanyabiashara wenye chapa zao kuzunguka ulimwenguni"amesema Nanai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Mwajuma Hamza amesema kuwa wanategemea wanawake asilimia 50 wataingia katika mradi huo na kuinuka na chapa zao.
Mshauri wa Mradi wa AFRAP Wambugu Wa Gichohi amesema kuwa mradi huo umekuja kuinua biashara kwa kukuza chapa 'Brand' na kuingia katika ushindani wa masoko nje Tanzania.
Julius Wambura akizungumza kuhusiana na mradi wa AFRAP wa kunuinua Biashara za wafanyabiashara wadogo katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Bw. Damas Mugashe akizungumza kuhusiana na mradi wa AFRAP wa kunuinua biashara za wafanyabiashara wadogo katika uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC), Mwajuma Hamza akizungumza kuhusiana na fursa hiyo kwa wanawake wafanyabiashara kuchangamkia katika uzinduzi mradi wa AFRAP Jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa mradi wa AFRAP Wambugu Wa Gichohi akizungumza namna Mradi utapotekelezwa na kuleta tija kwa Taifa,Jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...