Na Mwandishi wetu,Mbeya.

Vijana mkoani Mbeya wametakiwa kujikita katika shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali ili kukabiliana na changamoto ya ajira.

Ushauri huo umetolewa na mkurugenzi wa kampuni ya  Raphael group limited ambaye ni mzalishaji wa nafaka za mchele, unga wa sembe na maharage Raphael Ndelwa wakati akizungumza waandishi wa habari za utalii na uwekezaji wanawake wa Tanzania walioko mkoani hapo kwa ajili ya ziara.

"Niwashauri vijana wawekeze kwenye kilimo,fursa ipo kubwa kwa sasa kilimo kinalipa vijana waje huku sasa waje kuwekeza"amesema Ndelwa.

Mkurugenzi Ndelwa amesema kuwa serikali imetengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuweza kuijenga nchi kiuchumi mkoani mbeya.

"Nchi ya Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe,mimi kama mzawa nina omba watu tuendelee kuaminiana ili kuijenga nchi yetu"amesema Ndelwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...