Bw. Walney amekutana na
Mhe. Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo
mbili kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na utalii.
Amesema kukutana kwake na
Mhe. Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania
ambavyo vitamuwezesha kuwashawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza
katika sekta ya bishara na utalii nchini Tanzania
Kwa upande wake Mhe. Rais
Samia amemshukuru Bw. Walney kwa uamuzi wake wa kukutana nae na kujitambulisha
kwake na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na
Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.
Mhe. Rais Samia amesema
Serikali ya Uingereza na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa
muda mrefu ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini
Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika
kukuza ushirikiano wa uchumi na Uingereza.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Mhe Rais Samia ameshawasili Glasgow kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Wengine katika picha wa kwanza (Kushoto) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberatha Mulamula na wa kwanza (kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. PICHA NA IKULU.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...