WAFANYAKAZI 46 wa Kampuni ya Jandu constitution and Plumbing wamewasilisha maombi katika Mahakama Kuu Temeke kitengo cha Madai na Mirathi wakiiomba mahakama hiyo itoe mwengozo kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ili kuwalipa wafanyakazi hao mshahara yao wanayoidai kwa zaidi ya miezi 21 sasa.

Maombi hayo namba 495 ya mwaka 2019 ambayo leo Novemba 11,2021 yametajwa mbele ya Jaji Nyigulila Mwaseba yamefunguliwa na Folensi Kapara na wenzake 45.

Kwa mujibu wa hati ya maombi, pamoja na mambo mengine ,inadaiwa kuwa RITA aliteuliwa kuwa msimamizi wa Kampuni hiyo iliyokuwa ya marehemu Inderjit Singh Jandu.

Kwamba, waombaji ni wafanyakazi wa Kampuni hiyo mpaka sasa hivyo wanaiomba Mahakama Kuu imteue mtawala wa muda wa kuongoza Kampuni hiyo na kuwalipa mishahara yao ambayo hawajalipwa tangu Februari 2020 kwani mtawala aliyeteuliwa mpaka sasa RITA na tangu ateuliwe hajawahi kutimiza wajibu wake ikiwemo kuwalipa mishahara wafanyakazi kama alivyoelekezwa na Mahakama.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika kesi ya madai namba 634 ya mwaka 2019 wafanyakazi hao waliomba kupatiwa msimamizi wa muda kwakuwa aliyekuwa na jukumu hilo (Jandu ) alifariki Agosti 16 mwaka 2019.

Hivyo, baada ya mahakama kusikiliza maombi hayo, mahakama Kuu ilimteua mtawala wa muda kusimamia Kampuni ya marehemu ambaye ni RITA kwa ajili ya kukusanya na kulinda mali zote za marehemu, madeni, kulipa mishahara , kodi na mengine yote lakini hadi sasa wafanyakazi hao bado hawajalipwa mishahara yao

Hata hivyo, Kabidhi wasihi Mkuu wakili wa serikali Samwel Mutabazi alidai, Novemba 8, 2021 aliwasilisha pingamizi la awali mahakamani hapo akipinga maombi hayo kusikilizwa mahakamani hapo kwa kuwa haina mamlaka yabkufanya hivyo kwasababu shauri hilo ni linahusu masuala ya kazi hivyo linapaswa kusikilizwa mahakama ya kazi..

Pia amedai hati ya kiapo cha waombaji ni batili kwasababu hakionyeshi na tarehe wala saini zao za wapeleka maombi

Hata hivyo, Jaji Mwaseba ameomba.muda ili kupata maelekezo kutoka kwa Jaji Mfawidhi kwa sababu maombi hayo mbele yake yanatokana na kesi ya mirathi inayoendelea mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba24, mwaka huu ili kujua kama maombi hayo yatabaki katika mahakama hiyo au mahakama Kuu ambako kesi ya mirathi namba 70 ya mwaka 2019 inaendelea mbele ya Jaji Edwin Kakolaki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...