NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara ameutaka Wakala wa Majengo (TBA)kuboresha kitengo cha ufuatiliaji ili kujua nyumba ambazo zimekuwa zikipangishwa na kisha wahusika kuwapangisha watu wengine.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 17,2021 Jijini Dodoma katika ziara yake ya kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa na 150 zilizopo Nzuguni ambazo zinajengwa na Wakala huo kwa ajili ya watumishi wa umma ,Waitara Naibu amesema kuwa TBA wanawajibu wa kuboresha kitengo cha ufuatiliaji.

“Ule mpango mtu anapewa nyumba anakaa kisha onaondoka anapewa mtu mwingine bila makubaliano kama mkataba aliingia na watu wa TBA akitaka kuondoka ni lazima ukague nyumba wakati anaingia ilikuwaje na wakati anatoa imekuwaje.

“Nyumba zetu hizi ni nzuri lazima kuwe na kitengo cha kufuatilia kuona matengenezo yakoje,hili mtoe uzito.Lazima mboreshe kitengo cha ufuatiliaji mfano Dodoma mahitaji ni makubwa lakini wanataka pia nyumba iboreshwe,”amesema.

Aidha,Waitara ameipongeza TBA kwa kujenga nyumba bora na zenye kiwango kinachokubalika ambapo amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa tisa.

“Tunatarajia Rais atakuwa anafuatilia,bahati nzuri mnajenga nyumba na mitambo ya kokoto na matofali ipo hapahapa hakutakuwa na kisingizio.Nimefurahi mnafanya kazi na mradi utaisha mwakani mwezi wa tisa na viongozi wanatarajia kuzitumia nyumba hizi,”amesema

Kuhusiana na kwamba nyumba hizo kodi kuwa kubwa,Naibu Waziri Waitara amesema nyumba hizo ni za watumishi na zimejengwa na Serikali hivyo gharama zake zitakuwa ndogo.

“Nyumba hizi ni za watumishi na zimejngwa na Serikali ili kumpunguzia maisha mtumishi tukipangisha watumishi wakatosha tutapangisha watu wengine.,”amesema.

Vilevile,Waitara amemshukuru Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi Mkoani Dodoma.

“Kwanza nimshukuru sana Rais (Samia Suluhu Hassan) kwa kutoa fedha ametoa fedha nyingi kwa mfano pale nyumba 20 makisio ni shilingi bilioni 5 na ameishatoa fedha yote kwahiyo watu wa TBA kazi kwao tunatarajia nyumba zikamilike kwa wakati

“Eneo hili mnaloliona ni ekari 680 ni eneo kubwa tunakusudia kujenga nyumba za kawaida hizi zaidi ya 3000 katika eneo hili na zitakuwa nyumba za ghorofa.Kwa hiyo huu ni mradi mkubwa ambao tumeanza kama sehemu ya mfano tunatarajiwa watu wa TBA wakifanya vizuri zaidi Mheshimiwa Rais ataendelea kutoa hela,”amesema.

Kwa upande wake,Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma,Victor Balthazar amemshukuru Naibu Waziri kwa kutembelea mradi huo huku akiahidi watatekeleza kwa wakati mradi huo.

“Nataka nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kutembelea mradi wetu wa Kisasa na Nzuguni uliyoasema tutayazingatia na nikuahidi tuyafanyia kazi,Tutatekeleza kazi hii ndani ya muda ambao tumejiwekea na kujipangia lakini iwapo itatatokea changamoto tutatoa taarifa mapema ili tuweze kujua tutaitekelezaje,”amesema.

Vivile,ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo ambapo amedai kwa Mkoa wa Dodoma mahitaji ya nyumba kwa watumishi wa umma ni makubwa.

“Kama ulivyoeleza Mkoa wa Dodoma uhitaji wa nyumba ni mkubwa sana watumishi wengi hawana nyumba tunaishukuru Serikali kwa kuweza kutupatia fedha hizo tunaamini hatutamwangusha tutaitekeleza kazi hii kwa uadilifu,”amesema.

Amesema changamoto wanayokutana nayo kwa sasa ni kutokea kwa viashiria vya kuadimika kwa Saruji huku akidai suala la mchanga na kokoto wamelitatua.

“Tunajaribu tunakusanya mchanga mwingi na kokoto hata mvua itakapokuja tusipate shida kwani msimu wa mvua Dodoma huwa kunakuwa na shida jinsi ya kupata mchanga,”amesema.

Naye Mradi wa nyumba 20 za viongozi, Mkadiriji Majenzi Goddy Mduda amesema kuwa kati ya nyumba hizo zilizojengwa ni 19 Sawa na asilimia 50 ya kazi hivyo wapo kwenye umaliziaji.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa na 150 zilizopo Nzuguni zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) leo Jumatano Novemba 17,2021 Jijini Dodoma

Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma,Victor Balthazar,akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara, (hayupo pichani) mara baada ya kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa na 150 zilizopo Nzuguni zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) leo Jumatano Novemba 17,2021 Jijini Dodoma

Mradi wa nyumba 20 za viongozi, Mkadiriji Majenzi Goddy Mduda,akielezea ujenzi wa nyumba za Kisasa ulipofikia mara baada ya Naibu Waziri ,Mwita Waitara kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) leo Jumatano Novemba 17,2021 Jijini Dodoma.


Muonekano wa Mradi wa nyumba 20 za viongozi zinazojengwa na Wakala wa Majengo zilizopo eneo la Kisasa Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...