-Wanafunzi pamoja sekondari wakabidhiwa jezi mpya


NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO

Wanafunzi wa shule ya sekondari Pamoja iliyopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma imekabidhiwa jezi mpya kwa ajili ya timu yao ya mpira wa miguu shuleni Hapo.

Akikabidhi Jezi hizo Solomon Hyera alisema anatimiza ahadi yake aliyoihaidi wakati alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kwenye kumtangaza mshindi wa ligi ya mbuzi iliyofanyika shuleni hapo.

Hyera alidai aliahidi kutoa jezi kwa shule ya sekondari Pamoja kutokana na kujionea mwenyewe kuwa wanafunzi hao ni wapenda michezo lakini wanakosa jezi za kuvaa wakati wa michezo.

Lakini pia Hyera alitaja kitu kingine kilichomfanya kutoa zawadi hiyo ni kuwashukuru walimu wa shule hiyo kwa kumjali na kumpa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa ligi ya mbuzi iliyofanyika shuleni hapo.

Mwalimu wa michezo wa shule hiyo Azizi Mtumbey pamoja na kumshukuru Solomon Hyera kwa kutimiza ahadi yake aliwata wanafunzi kujituma kwenye michezo kwani michezo ni Sanaa,taaluma na ajira .

Mkuu wa shule ya Sekondari Pamoja Amos Mapunda pamoja naye alimshukuru Hyera kwa kutimiza ahadi yake na alimwomba kuendelea kuisaidia shule hiyo kwani inachangamoto nyingi .

Mapunda alidai kuhaidi kutoa zawadi na kutimiza ahadi yako ni moyo wa uzalendo na upendo ulionao kwa shule ya sekondari ya pamoja alisema mapunda.

Aliwataka wadau wengine wenye moyo kama wa hyera kujitokeza kusaidia shule hiyo kwani inachangamoto za miundombinu ya uhaba wa madarasa,mabweni,maabara,nyumba za walimu ,bwalo la kulia chakula pamoja na makataba.

Shule ya sekondari ya Pamoja ni shule ya kidato cha tano na sita kwa wavulana iliyojengwa wilayani Namtumbo kwa michango za halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma ambapo kwa sasa shule hiyo inachangamoto za miundombinu licha ya wanafunzi kufanya vizuri kitaaluma.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...