Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.
Spika
Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na
kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa
viongozi.
Ndugai
ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni
alipokuwa akizindua mafunzo ya uongozi kwa wabunge wanawake.
Mafunzo
hayo yameandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa lengo la
kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi. Spika amesema Taifa
linaloongozwa na mwanamke linakuwa tulivu , amani na salama.
"Lakini
kauli za baadhi zinaharibu taswira nzima, wengine mavazi yenu yanakuwa
ya hovyo, ukipewa cheo kazi yako inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani
jambo linaloharibu taswira ya viongozi wakuu wa nchi," amesema Ndugai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...