Watalii wakiwa kwenye magari ndani ya Hifadhi ya Mikumi.
KUNDI la Watalii 62 kutoka nchi za Urusi, Ubelgiji, Ukraine, Uswisi, Poland na Ujerumani leo asubuhi wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa ajili ya kuvishuhudia vivutio vya utalii vilivyopopo ndani ya Hifadhi hiyo. Haya ni matokeo ya juhudi mbalimbali za utangazaji zinazoendelea kufanywa na Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi.
Watalii wengi wanaendelea kuonesha kuwa na imani na Tanzania kwa hatua stahiki zinazochukuliwa dhidi ya mapambano ya UVIKO 19. Bodi yaUtalii inaendelea kuwahimiza wadau wote wanaihudumia watalii kuendelea kuzingatia taratibu za kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19 ili kuwavutia watalii wengi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...