Mgeni
rasmi wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, Waziri wa
Nchi Afisi ya Rais , Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mhe. Jamal K. Ali, alipotembelea katika banda la Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF). Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa
yanaendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo NSSF inaendelea kutoa
elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba
akipata maelezo kutoka kwa Afisa matekelezo mwandamizi Hawa Godigodi,
alipotembelea banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za
Fedha kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Masha Mshomba
akielezea huduma mbalimbali zinazotelewa na NSSF katika maadhimisho ya
Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. Katika maadhimisho hayo NSSF inatoa
elimu kuhusu hifadhi ya jamii, elimu kuhusu umuhimu wakujiwekea akiba,
elimu ya huduma zinazotolewa kwa njia ya mtandao ambapo ndio
kipaumbele muhimu cha Mfuko pamoja na kueleza fursa za uwekezaji.
Mkurugenzi
wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu, Festo Fute
(katikati) akisisitiza jambo alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za iFedha
kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, kulia ni Meneja Uhusiano na
Elimu kwa Umma, Lulu Mengele pamoja na wafanyakazi wa NSSF
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma (kulia),
akipata maelezo mbalimbali kuhusu ushiriki wa NSSF katika Maonesho ya
Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa. Maonesho haya yanaendelea katika
viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba
akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais , Fedha na Mipango,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali kuhusu huduma
mbalimbali zinazotolewa na NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za
Fedha kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba (wa
kwanza mstari wa mbele) akiwa katika ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya
Huduma za Fedha Kitaifa, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam
Waziri
wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya
pamoja na Kamishna Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha
Dkt. Charles Mwamwaja (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni
aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Fatma Nyangasa na
viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba,
akiwa katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ambapo
alipata fursa ya kutembelea na kupata maelezo katika banda la Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Mifuko hiyo ipo katika
viwanja vya Mnazi mmoja kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali
zinazotolewa kwa wanachama wao.















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...