Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
SERIKALI
kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa maadhimisho ya wiki ya
huduma ya fedha kitaifa ambayo yatafanyika Novemba 8 hadi Novemba 11
mwaka huu lengo likiwa kujenga uelewa na weledi kwa umma katika
matumizi sahihi ya huduma za fedha zinatolewa.
Akizungumza wakati
akifungua semina ya siku moja kwa wahariri wa vyombo mbali mbali vya
habari nchini kuhusu masuala ya fedha na maadhimisho ya wiki ya huduma
za fedha kitaifa ,Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango ndugu Emmanuel
Tutuba amesema katika wiki hiyo Wizara imejielekeza katika masuala
mbalimbali yakiwemo kuimarisha ufanisi wa masoko ya fedha kupitia elimu
ya fedha,kuongeza upatikanaji wa huduma za fedha.
‘’Hatutaishia
hapo tutatoa elimu ya kuwezesha kumlinda na mtumiaji wa huduma za
fedha,kuwezesha wananchi kusimamia vizuri rasilimali fedha,kuwawezesha
wajasiriamali wadogo kuongeza ujuzi na matumizi sahihi ya huduma za
fedha katika kukuza biashara zao,kuimarisha utamaduni na kujiwekea
akiba,kukopa na kulipa madeni na kuongeza mchango wa sekta ya fedha kwa
ukuaji wa uchumi,’amesema.
Aidha ametoa mwito kwa vijana
kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo katika kujifunza kwa kuwa
sekta hiyo imejipanga kuwahudumia vizuri ili kuwawezesha kutizama na
kuchangamkia fursa katika wizara hiyo.
Ameongeza Wizara hiyo
imejipanga vizuri kuhakikisha inatatua changamoto ikiwemo ya uelewa
mdogo wa masuala ya fedha,uelewa mdogo wa bidhaa zitolewazo na watumiaji
na watoa huduma za fedha,matumizi ya huduma za fedha zisizo
rasmi,ambapo utekelezaji wa programu hiyo inakusudiwa ifikapo
2025,takribani asilimia 80 ya wananchi wawe wamepata uelewa wa masuala
ya fedha.
Maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es
Salaam na kubebwa na kauli mbiu isemayo ‘’Boresha Maisha kupitia Elimu
ya Fedha’’.
Katibu
Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel
Tutuba akizungumza leo Novemba 1,2021 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi
wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi wa habari kwa
ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya Fedha na maadhimisho ya wiki
ya Huduma za Kifedha Kitaifa inayotarajiwa kuanza Novemba 8-14 katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu kwenye
maadhimisho hiyo imetajwa kuwa ni ‘Boresha Maisha kupitia Elimu ya
Fedha’.
Kamishna
Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Dkt. Charles
Mwamwaja akitoa maelezo ya kikao kazi hicho kabla ya kufunguliwa kati ya
Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali nchini,
Kikao hicho pamoja na mambo Kadhaa kinajadili kuhusu Sekta ya Fedha na
Maadhimisho ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa ambacho kinafanyika
kwenye ukumbi wa Kambarage Ofisi ya Hazina jijini Dodoma.
Kaimu
Kamishna Msaidizi Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Dionisia
Mjema akisikiliza maswali kutoka kwa washiriki wa mkutano huo mara baada
ya kuwasilisha mada yake kuhusu Wasilisho la Mpango Mkuu wa Maendeleo
ya Sekta ya Fedha.
Kaimu
Kamishna Msaidizi Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Jannet Hiza
akitoa mada kuhusu Programu ya Kutoa Elimu kwa Umma ya Mwaka
2021/22-2025/26.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu Serikali Bw. Emmanuel Tutuba kulia
,Kamishna Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja
pamoja na Kamishna Msaidizi Wizara ya Fedha Dionisia Mjema
Afisa
Uhusiano, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Bi. Asha Hussein
Saleh (kushoto) na Bw.Salim Kimaro, Afisa Msimamizi Mkuu wa Fedha, Idara
ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha
Baadhi
ya maafisa habari kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na
Mipango wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kweye mkutano huo.Baadhi ya Wahariri wa Habari wakifuatilia mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja akitoa ratiba na miongozo mbalimbali katika mkutano huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...