Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Mnamo tarehe 17, March 2016 Serikal ilitoa tamko la kuzuia ukamatajivna usafirishaji wa WANYAMAPORI hai nje ya nchi baada ya hatua hiyo Serikal iliamua kuwarejesha wafanyabiashara wa WANYAMAPORI hai kiasi cha shilingi 173,289,430.60 ikiwa ni ada mbalimbali walizolipa kabla ya kusitishwa kwa biashara hiyo.
Hayo yamezungumzwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Merry Masanja wakati akisoma taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma.
Aidha Naibu Waziri huyo amesema katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara wizara iliunda kamati ya wataalamu kwa ajili ya kufanya tadhimini ya biashara ya kusafirisha WANYAMAPORI hao.
Aidha Serikali imesema utaratibu huo utakapoanza kutumika pamoja na kuwezesha wafanyabiashara hao kuwekeza zaidi kwenye ufugaji wa wanyamapori pia utasaidia kulinda sekta hiyo ya utalii kwa kuendelea kuwavutia wageni kuja nchini kuona wanyamapori hai wakiwa kwenye mazingira yao ya asili. Na utaratibu mpya utapunguza gharama za kuhifadhi wanyamapori hai na pia mnyororo wa biashara hiyo utaweza kuwanufaisha watanzania wa makundi yote kuanzia wategaji (trappers), wataalamu wa kuchakata nyara na wasafirishaji wenyewe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...