Linkee, kampuni mpya ya kiteknolojia yatangaza mchakato wake wa usajili wa madereva Dar es Salaam na kuwakaribisha madereva wote kujiunga mapema kwenye programu yao ili kufurahia faida nyingi za kipekee. Mwaliko huu ni kwa ajili ya madereva wa magari, pikipiki na bajaji.

Linkee inajiandaa kufanya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam, ambapo kampuni hii mpya inalengo la kufanya mapinduzi kwenye ujasiriamali, usafiri na katika uchumi wa kugawana.

Kutokana na kwamba Dar es Salaam ni soko la uzinduzi la kampuni hii, Linkee inataka kutengeneza muamko wa nguvu kwa madereva kupitia nafasi hii ya kipekee kwenye soko ya kutoa mapato yote kwa miezi 6 baada ya uzinduzi kwa ajili ya madereva waliojisajili kwenye programu. Hakuna pingamizi au vizuizi au idadi ya safari zinazohitajika. Mpango huu utawahamasisha madereva kutumia Linkee, wakijua ya kuwa asilimia 100 ya faida kutoka kwenye safari zao itaenda mfukoni mwao.

Faida yote itaenda kwa madereva ambapo Linkee itatoa orodha ya safari na bei ambayo madereva watachagua kutokana na mipango yao. Linkee haitaomba idadi fulani ya safari kufanyika ndani ya siku au masaa ya kufanya kazi kwenye hii programu na haitatoa adhabu kwa dereva pale ambapo muafaka hautopatikana. Madereva wana uamuzi wa  jinsi ya kutengeneza faida zao.

Timu ya Linkee yenye jukumu la kutengeneza fursa hiyo imesherehekea hatua hii muhimu: Wana fahari kubwa kuitambulisha Linkee kwa ulimwengu mzima kupitia uzinduzi ujao jijini Dar es Salaam. Wanaleta Linkee Tanzania kwa ajili ya Watanzania, na wanaamini ahadi yao ya kuboresha mapato ya madereva na kujenga jamii ya kugawana na usafiri wa kirafiki, wenye ufanisi na rahisi ni njia sahihi kwa kampuni ya Linkee. kila senti itahesabika kwa ajili ya madereva na watumiaji wengine na pia tunaamini sasa ni wakati wa teknolojia kupatikana kirahisi ili kuboresha jamii na kukuza ubora wa maisha wa kila mmoja. "Hilo ndilo lengo la Linkee".

Linkee itakuwa na program ya usalama  ambapo kila safari itatoa huduma ya usalama ili madereva na watumiaji waweze kutuma safari zao kwa watu wanao waamini na kama kuna uhitaji wanaweza kutoa taarifa polisi moja kwa moja. Linkee inataka kusherekea umoja na mshikamano  kupitia program hii na kutathmini safari ili watumiaji waweze kusoma maoni, mapendekezo na maswali.

Jinsi ya kujiandikisha na Linkee
Ni programu rafiki na rahisi. Na vifuatavyo ni vitu 6 ambavyo madereva wanatakiwa kupakia kwenye programu ya Linkee moja kwa moja:

Madereva:

1.- Leseni ya udereva

2.- Picha ya Wasifu

3.- Picha ya uthibitisho wa kitambulisho

 

Magari:

4.- Usajili wa gari

5.- Bima ya gari

6.- Picha ya uthibitisho wa gari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Habari zenu, nipo hapa kushuhudia, jinsi nilivyo kuwa mwanamitindo tajiri na maarufu duniani mwenye mafanikio makubwa, nimekuwa nikipitia magumu miaka nenda rudi, tangu nilipofiwa na wazazi wangu wote wawili, sikuweza kuendelea zaidi na mshikaji wangu kutokana na Suluhu la kifedha basi, hadi miezi mitano iliyopita, nilimaanisha rafiki ambaye aliniingiza kwenye familia ya freemason, mwanzoni niliogopa kujiunga, kwa sababu nimesoma habari nyingi za uongo kwenye mtandao kuhusu familia ya freemasonry, na ambayo sasa ninaijua. hiyo sio kweli, zote zilikuwa habari za uongo, na napenda kutumia fursa hii kusema asante sana kwa familia ya freemason, ndugu wote wa familia hii, nawashukuru sana kwa support mnayonipa, na kwa waliodhani familia ya freemasonry ni mbaya, haijui sheria na kanuni za huyu jamaa, tafadhali acha kuhukumu ulikuwa hujui, na acha kusambaza habari za uongo, kama una nia ya kuwa mwanachama ufurahie. faida za familia ya freemasonry, contact off anuani icial hapa chini kwa taarifa zaidi.

    WhatsApp; +31 687 329 133
    Barua pepe; info.masonic.oregon@email.cz
    Barua pepe; info.masonic.oregon@gmail.com
    Au soma zaidi kuhusu sisi kwenye kiungo cha ukurasa wa Facebook; https://web.facebook.com/infomasonicoregon

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...