*****************

Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekuwa Mshindi wa kwanza na kupata tuzo mbili za taasisi iliyoandaa vizuri taarifa za mahesabu kwa mwaka 2020.  

Tuzo ya kwanza ni katika Kundi la Wizara na Idara zinazojitegemea (MDAs) za Kiserikali iliyo andaa vizuri  Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa Sekta ya Umma (IPSAS) kwa mwaka huo na ya pili ni ya Mshindi wa jumla kwa MDAs zinazotumia IPSAS.

Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo Gerald Musabila Kusaya wakati akipokea tuzo hizo, ameeleza kuwa, mbali na Mmlaka kuweka mkazo katika kutekeleza majukumu yake ya udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya  bado imekuwa na umakini mkubwa katika kusimamia matumizi ya fedha.            

Aidha, ameeleza kuwa, umakini huo ndiyo umeifanya Mamlaka kuendelea kupata ushindi huo mfululizo  ambao ni wa nne sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...