Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart Scolastika Kevela akikabidhi zawadi kwa uongozi na watoto wa kituo cha Jeshi la Wokovu ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii na kusherekea sikukuu za mwaka na wenye uhitaji.
KAMPUNI Ya Udalali ya Yono Auction Mart imetoa msaada wa vyakula kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa katika kituo cha Jeshi la Wokovu ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii na kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ambazo kampuni hiyo hushiriki na wahitaji mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart na Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM,) Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amesema kampuni hiyo imekuwa ikisherekea sikukuu za mwisho wa mwaka na wahitaji na kutoa misaada muhimu ikiwa sehemu ya kurudisha kwa jamii kwa kile walichokipata kupitia huduma wanazotoa kwa jamii.
"Watanzania tulio ndani na nje ya nchi tuangalie wenye uhitaji hasa watoto, tuje tushiriki nao kwa kile tunachokipata na nimeona hapa wamefurahia zawadi tulizowaletea." Amesema.
Amesema, watanzania ni vyema wakaendeleza ukarimu kwa kuwakumbuka watu wenye uhitaji ili kuacha alama katika jamii.
"Watumishi na watoto wa kituo hiki naomba mtuombee katika shughuli zetu za kila siku na tutaendelea kurudi hapa kila wakati.....watumishi wa hapa Mungu awabariki kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwalea watoto hawa." Amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Jeshi la Wokovu Mary Nyika amesema kuwa kujitokeza kwa wadau wa namna hiyo ni kuisaidia Serikali ambayo imekuwa ikibeba majukumu ya watoto hao.
Amesema kuwasaidia watoto hao ni baraka na kuwaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada za Yono kwa kuwasaidia watoto hao.
"Shule hii ina wana wanafunzi 220 ambao ni walemavu wa viungo na wenye ualbino, Serikali imekuwa ikitoa msaada kwa kiasi kikubwa sana, Tunawashukuru Yono kwa msaada huu tunawaombea na Mungu awabariki." Amesema.
Yono Auction Mart imetoa msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo mchele, sabuni, vinywaji, sabuni, pamoja na mbuzi kwa ajili ya kusherekea sikuuu ya Krismasi.
Mmoja ya watoto wa kituo hicho akitoa shukrani kwa uongozi wa Yono Auction Mart kwa msaada waliowapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...