Na Farida Said, MiCHUZI TV.
HALMASHAURI ya Baraza Kuu la Waisilamu Tanzania BAKWATA Mkoa wa Morogoro imemsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Baraza hilo Mkoa wa Morogoro Ustadhi Ahmad Heirallah kutokana na ukiukwaji wa maadili ya uongozi.

Taarifa ya kusimamishwa kazi kiongozi huyo imetolewa na Kaimu Sheikhe Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA Mkoa wa Morogoro Sheikhe Twaha Kilango baada ya kikao cha baraza la mashekhe Mkoa wa Morogoro.

Aidha amesema baraza halitomvumilia na kusita kumchululia hatua mtu yeyote atakayekiuka maadali ya uongozi wa dini hiyo na kuwataka waumini kuwa na imani na viongozi wao.

Hata hivyo Sheikhe Kilango amesema Halmashauri ya BAKWATA Mkoa wa Morogoro imemteua Ustadhi Muhammad Bafadhwili kukaimu nafasi hiyo hadi taratibu za kumpata katibu zitakapokamilika.

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo kaimu katibu wa BAKWATA Mkoa wa Morogoro Ustadhi Muhammad Bafadhwili amelishukuru baraza hilo kwa kumuamini na kumchagua kushika nafasi hiyo na kuwaongoza waislamu wanzake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...