SHAHIDI wa 12 wa upande wa Jamhuri katika Kesi ya uhujumu uchumi yenye Mashtaka ya Ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadem Freeman  Mbowe na wenzake watatu ameileza mahakama kuwa Mbowe alimuomba amtafutie Makomandoo ili nchi isitawalike.


namna ambavyo  waliwasiliana na Mbowe  ambaye alimweleza Mipango  aliyonayo ili Nchi Isitawalike.


 Shahidi huyo ambaye ni ofisa wa Jeshi la  Wananchi Tanzania JWTZ Luteni Urio  ambaye  kituo chake cha Kazi ni kikosi namba 92 cha Jeshi cha KJ cha Makomando Kilichopo  Ngerengere Mkoani Morogoro ameeleza hayo leo Januari 26,2022  mbele ya Jaji Joachim Tigangab wa mahakama Kuu kitengo cha Mafisadi.

Akiongozwa na Wakili wa serikali Mwandamizi Abdallah Chavula, Urio amedai kuwa, alijiunga  na JWTZ June  16 mwaka 2003,  akiwa Luteni ambaye majukumu yake yalikuwa ni  kuwasimami Askari waliopo chini yake na Pia kutoa mafunzo kwao


Alipoulizwa ni namna gani alifahamiana na washtakiwa Khalfan Bwire, Adam Kasekwa maarufu Adamoo, Mohamed Ling'wenya  na Freeman Mbowe na kama anawafahamu aliwafahamu Vipi.

Akijibu hayo amedai aliwafahamu washtakiwa hao kwa namna tofuati tofauti na kwamba, Khalfan  Bwire anafahamiana naye  tangu  mwaka  2006 hadi 2019 kwa sababu  amefanya nae kazi na ndiye alimpa mafunzo ya ukomando huku Bwire alimfahamu kama Koplo ambaye ajira yake ilikoma jeshini mwaka 2019 baada ya Kufukuzwa kutokana na Utovu wa Nidham  na Pia Muda wote   wa utumishi wake  yeye alikuwa Kiongozi Mdogo.


 Ameda Kuwa Kipindi Bwire anafukuzwa kazi yeye alikuwa Darful Sudan na aliporejea nchi alipewa taarifa na Utawala Kuwa Bwire amefukuzwa kutokana na Utovu wa Nidhamu.

  
 Amedai kuwa, anawafahamu Adam kasekwa na Mohamed  Ling'wenya kwa sababu nao pia alikuwa anafanya nao kazi jeshini kikosi  92 Ngerengere Morogoro na wote walifukuzwa Jeshini kutokana na Utovu wa nidhamu.

 Ameongeza kudai kuwa, kipindi chote alipokuwa kazini mahusiano yake na washtakiwa yalikuwa mazuri na hata baada ya kufukuzwa kazi waliendelea kuwasiliana.

Akieleza namna alivyofahamiana na Mbowe, Uria amedai,  alifahamiana na Mbowe kuanzia mwaka 2008 hadi 2020 na nam kwamba anakumbuka Alipigiwa simu kwa namba ngeni ikimuuliza we ndo Denis Urio Askari wa JWTZ   akaitikia na yeye ndipo mpigaji wa simu akajitambukisha kwa Jina la  Freeman Mbowe.
 
 Amedai katika maongezi yao, Mbowe alimuuliza kuwa "wewe si wa Kilimanjaro Urio akamjibu ndio  ndipo Mbowe akamjibu kuwa tunatakiwa kufahamiana huku Urio akimhoji kwenye Simu kuwa namba yake kaipata wapi  na Mbowe alimwambia  kitaka namba ya Mtu yeyote anapata  hivyo asiwe na wasiwasi.

Urio amedai baada siku hiyo,  Mbowe akawa anamtumia ujumbe wa maandishi kumpa heri ya sikukuu pindi ikitokea.


Amedai kuwa katika mahusiano yao ya muda mrefu, mwaka 2012 walikuja kukutana ana kwa ana baada ya yeye kurejea Nchini akitokea Darful Nchini  ambako alikuwa kwa ajili ya kulinda amani.


Amedai, katika mwaka huo huo, siku moja Mbowe alimpigia simu na kumuuliza kama wanaweza kuonana Mikocheni katika Hotel Cassa jambo ambalo alilikubali ingawa hakuwa akipafahamu hapo mahali ndipo Mbowe alimwelekeza kuchukue Tax ili imfikishe mahali hapo naye alifanya hivyo.

Amedai baada ya kufika pale, Mbowe ndiye alilipia taksi ile kiasi cha sh. 20,000.

 Amedai katika maongezi yao Mbowe alimueleza mambo matatu ambapo kwanza alitaka kujua yeye ni nani cheo chake na  mahali anapofanyia kazi na  alimjibu kuwa anafanya kazi Morogoro na Nyumbani kwake ni  Kilimanjaro.

 Pia amedai  Mbowe  alitaka kujua msimamo wake  dhidi ya chama cha Upinzani na akamjibu kuwa  kwa  taratibu wa kazi yake  haruhusiwi kufungamana na Chama chochote Ila kwa kiongozi aliyepo madarakani


 Jambo la  tatu ambalo alimuuliza ni kama kulikuwa kuna makampuni yanayofungua mfumo wa  mawasiliano jeshini ndipo na yeye akamuuliza kwa nini alikuwa akitaka  jeshi likafunge mawasiliano  kwenye ofisi Mbowe akamjibu kuwa anataka afanye hivyo ili awafuatilie viongozi  wa Chadema wanaotoa siri za chama nje.

Amedai, alimshauri aende kwenye  taasisi za Elimu ya Juu kisha yeye anaondoka na akampa hela ya Tax ya kumrudisha pale ilipomtoa.

Amedai kuwa baada ya Makutano ya siku hiyo mawasiliano yalikuwa yanaendelea Kama kawaida na  Mbowe ndie alikuwa anamtakia kheri za Sikukuu ambazo zinakuwepo kwa wakati Huo.

Amedai,  May 7,  2020 walikutana kwa mara nyingine katika Mgahawa ambao amedai  haukumbuki Jina,  Mikocheni Dar es  Salaam akimueleza kuwa alikuwa kuna masuala  ya kuzungumza na alifanya hivyo na Mbowe alizoea kumwita Jina La Homeboy.

"Homeboy mwaka huu 2020 kuna uchaguzi mkuu na chama changu kimepanga Kuchukua Dola kwa namna na Kwa gharama yoyote Ile.....  si  unaona watu wa chini na wanyonge wanavyoishi maisha ya Shida",


 Urio amedai Mbowe alimwambia  amtafutie  vijana ambao watamsaidia katika kuambatana nae ili Ili kufanya mambo ambayo yatafanya nchi isitawalike Ikiwa ni pamoja na  kulipua vituo vya mafuta, kukata miti mikubwa na kuiweka barabarani Ili isipitike na pia Kuwadhuru viongozi wa serikali ambao wanazuia harakati za Chama akiwemo aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Olesabaya.


 Amedai  baada ya kurudi nyumbani  alishindwa kukaa na zile taarifa na usiku ule wa saa tatu akampigia  simu Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI na kumwelezea  Mazungumzo yake na Mbowe ndipo DCI akamtaka kesho yake afike ofisini  kwake na Alifanya hivyo.

Baada ya mazungumzo yangu na DCI alinishauri niendelee  na taratibu za kumtafutia makomando hao na nitoe taarifa kila hatua ninayoipitia ndipo nilimtafutia vijana wawili ambao  Mose Lijenje na Khalfan Bwire  na baadae nilimpa taarifa  Mbowe  na aliniambia niendelee kutafuta kuwa vijana wengine, baadae nikampata Ling'wenya  yeye akampigia Rafiki yake Adam Kasekwa.

Kesi hiyo itaendelea kesho..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...