GARI la waandishi wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi. Robert Gabriel Luhumbi limepata ajali eneo la Busega walikuwa wakielekea Ukerewe kwa kupitia Bunda leo Januari 11, 2022.
Mwenyekiti Mwanza Press Club, Edwin Soko , ameongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akitoa taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki dunia.
Majina ya walioariki dunia yatatolewa kadri itakavyofuatiliwa.
"Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.
Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati timu yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo."
Baadhi ya wananchi wa eneo la Busega wakiangalia ajali iliyotokea mapema leo Januari 11, 2022.
Gari lililokuwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mkoani Mwanza.
Gari dogo aina ya haice iliyopata ajali kwa kugongana uso kwa uso na Gari lililokuwa na waandishi wa habari mkoa wa Mwanza leo Januari 11, 2022 katika eneo la Busega jijini Mwanza.
UPDATES.........................................................
Waandishi ambao wamethibitishwa kufariki dunia ni Waliofariki ni
1.Husna Milanzi - ITV
2.Johari Shani - Uhuru Digital
3.Antony Chuwa - Freelancer
4.Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
5.Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.
Majeruhi.
1.Tunu Heman - Freelancer
2 Vany Charles - Icon TV
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...