Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI
ya JK White Cement, Tanzania imeendelea kutambua mchango wa Wadau wake
waliopo sehemu mbalimbali nchini kwa kuwakabidhi zawadi mbalimbali baada
ya kufanya vizuri katika matumizi ya bidhaa zao kupitia promosheni
maalum ya Faidika na Bidhaa mpya ya JK Wall Putty iliyotambulishwa mwaka
2021.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo na Masoko wa
Kampuni hiyo, Felista Masabo amesema wametoa zawadi hizo ili kuthamini
na kutambua mchango wa Wadau wake ambao ni Wauzaji, Wanunuaji na
Watumiaji waliopo sehemu mbalimbali nchini.
Masabo
amesema lengo kubwa la kutoa zawadi hizo ni kuwapa mkono wa ahsante
sambamba na kuwashukuru kwa mchango wao Wadau hao katika matumizi ya
bidhaa zao sanjari na kugawana kinachopatikana kupitia bidhaa hizo.
“Watumiaji
ambao ni Mafundi Rangi, tumewazawadia zawadi kwa kutambua mchango wao
kwetu, wametuunga mkono, na kututhamini, tunaamini wao ni Wadau wetu
tunataka, sisi tupate na wao wapate, pia tunataka kila anayetumia bidhaa
zetu awe mshindi”, amesema Masabo.
Kwa
upande wao Washindi wa Promosheni hiyo wamesema bidhaa za JK White
Cement ni nzuri kwa matumizi ya ujenzi, zimewasaidia kwa kiasi kikubwa
katika shughuli zao za ujenzi.
“Natumia
sana bidhaa zao (JK White Cement) zinatoa Fangasi za ukutani kwa kiasi
kikubwa, mara kwa mara huwa natumia na inapendezesha ukuta”, amesema
Yassin Yassin.
Washindi
hao watatu wamepatikana kupitia Promosheni hiyo ya JK Wall Putty
iliyoanzishwa mwaka jana, Washindi hao ni Yassin Yassin kutoka mkoa wa
Mwanza, ambaye amezawadiwa Jokofu, mshindi wa pili ni Weston Komba
kutoka Dar es Salaam amezawadiwa Runinga na vifaa mbalimbali vya ujenzi
na mshindi wa tatu Michael Ernest kutoka mkoa wa Dodoma ambaye
amezawadiwa Radio kubwa (Subwoofer).
Meneja
Mauzo na Masoko wa Kampuni ya JK White Cement, Tanzania , Felista
Masabo akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wakitangaza Washidi
watatu kutoka mikoa mbalimbali nchini wa Promosheni ya ya Faidika na
Bidhaa mpya ya JK Wall Putty, hafla hiyo ya ugawaji wa zawadi hizo
ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa JK White Cement, Manish Shrivastava akikabidhi zawadi kwa Mshindi wa
kwanza wa Promosheni ya Faidika na Bidhaa mpya ya JK Wall Putty
iliyoanzishwa mwaka 2021 kwa lengo la kutambua, kuthamini mchango wa
Mafunzi Rangi kupitia bidhaa za Kampuni hiyo kwa wadau wake, wa kwanza
kulia ni Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya JK White Cement, Tanzania,
Felista Masabo akishuhudia.Picha
ya pamoja kati ya Wafanyakazi wa Kampuni ya JK White Cement, Tanzania
na baadhi ya Wauzaji, wanunuaji na watumiaji wa bidhaa za Kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...