CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ametoa ufafanuzi juu ya tukio la kupigwa kwa mtu mmoja katika mazingira ya chuo hicho tarehe 23/01/2022.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Chuo cha NIT, Prof. Enjinia Zacharia Mgalimwa, imesema tukio hilo limeleta taharuki kubwa miongoni mwa wadau wa chuo na jamii kwa ujumla, hivyo uongozi umelazimika kutoa ufafanuzi huo.  

Taarifa hiyo imesema, ni kweli tukio hilo lilitokea chuoni na aliyekumbwa na kadhia hiyo siyo mwanafuzni wa chuo cha NIT bali ni mfanyakazi anayefanya kazi katika mojawapo ya kampuni iliyopo chuoni anayeitwa Happy Diamond.

Pia imeeleza suala la ulinzi wa chuo , kuna mzabuni aliyepewa kazi hiyo ambaye ni SUMA JKT, kwa hiyo aliyefanya tukio lile sio mtumihsi wa NIT bali ni mmoja wa wafanyakazi wa SUMA JKT.

Baada ya tukio hilo Uongozi wa Chuo umechukua hatua ya kutoa onyo kwa kampuni ya ulinzi husika kuhusiana na tukio hilo la kutumia nguvu kwa wadau wa chuo. Pia kampuni ya SUMA JKT imewachukulia hatua za kinidhamu wahusika wote ikiwemo kuwaondoa kazini.

Taarifa hiyo imesema, uongozi wa chuo utaendelea kusimamia taratibu na kanuni za mavazi kama miongozo ya utumishi wa serikali inavyoelekeza ili kuwalea vijana wetu katika maadili stahiki bila ya kuleta taharuki kwa umma.

Mwisho uongozi wa chuo cha NIT unatoa pole na kumuomba radhi umma kwa taharuki iliyojitokeza na kuahidi kuendelea kufuatilia utendaji wa SUMA JKT ili kuhakikisha suala kama hili kutokujiruka tena.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...