Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo leo Jumanne Januari 11, 2022 amewasili Zanzibar kwa ajili ya kushiriki sherehe za kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Afadhal Taib Afadhal

Sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar zitafanyika kesho tarehe 12 Januari, 2022 Katika uwanja wa Amani Zanzibar.

Imetolewa na;


Said Said Nguya

Afisa Habari

Ofisi ya Katibu Mkuu

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...