Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mwanasheria wa mkoa wa Njombe wakili Hilmar Danda amewataarifu wananchi wa mkoa huo juu ya mabadiliko ya sheria ya sheria NO 5 ya mwaka 2021 kwenye mabaraza ya ardhi na kubainisha kuwa mabadiriko hayo yamefanyika kwa lengo la kuboresha ufanyaji kazi wa mabaraza hayo.

Aidha amesema sheria hiyo imepiga marufuku kwa mabaraza ya kata kufanya kazi ya kusuruhisha migogoro katika maeneo yoa zaidi ya siku 30

“Sheria hii ya mabadiriko inataka baraza la kata lifanye kazi ya kupatanisha ndani ya siku 30 sio kesi inaenda kwenye mabaraza miezi miwili hiyo ni marufuku.Na kama endapo siku 30 zimepita hajafikiwa mwafaka kesi inaruhusiwa kwenda kufunguliwa kwenye baraza la ardhi wilaya kwa maelezo”alisema wakili Hilmar Danda

Aidha amesema mabadiriko ya sheria hiyo yametokana na changamoto mbali mbali zilizokuwa zikitokea kwenye mabaraza ya kata

“Ilionekana wazee wa mabaraza wanatoa hukumu wakati wao sio wanasheria.Kwa sasa sheria inawataka waishie kusuruisha tu migogoro na kesi itaanza kuhukumiwa kwenye baraza la wilaya” aliongeza Hilmar Danda

Vile vile amesema maamuzi mengi yaliyokuwa yakitolewa na mabaraza ya wilaya yakikiuka sheria za nchi

“Maamuzi mengi yaliyokuwa yanatolewa na mabaraza ya kata yalikuwa yanakiuka sheria za nchi,ili kutatua hiyo Changamoto kubwa serikali imeona kesi hizo kutolewa na mabaraza ya wilaya.Mabaraza ya kata yamebakiwa na kazi ya kusikiliza na kupatanisha”alibainisha Hilmar Danda mwanasheria wa mkoa wa Njombe

Kwa upande wake wakili Izack Mlowe amabye ni hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Njombe,ametoa wito kwa jamii kuendelea kufuatilia elimu mbali mbali zinazotolewa na serikali kwa kushirikiana na mawikili juu ya maswala ya sheria ili kupunguza changamoto zinazotokana kukosa elimu za kisheria.
Mwanasheria wa mkoa wa Njombe wakili Hilmar Danda,akionyesha mfano wa Tangazo la mabadiriko ya sheria yaliyobandikwa kwenye maeneo ya upatikanaji wa haki ili wananchi waweze kutambua mabadiriko hayo.

Mwanasheria wa mkoa wa Njombe wakili Hilmar Danda,akitoa taarifa ya mabadiriko ya sheria ya sheria NO 5 ya mwaka 2021 kwenye mabaraza ya ardhi ili wananchi jamii iweze kutambua mabadiriko ya sheria hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...