Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 11 Januari 2022 akiwa nchini Malawi amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Dharura wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit) pamoja na Jamhuri ya Msumbiji na nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji.
Akifungua mkutano huo mwenyekiti wa Troika ambaye pia ni Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza umuhimu wa kuiunga mkono Jamhuri ya msumbiji katika mapambano yake dhidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayoendelea katika Jimbo la Cabo delgado Kaskazini mwa Msumbiji.
Amesema ni muhimu Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) kushirikiana katika kuimarisha ulinzi na usalama na kurejesha hali ya Amani na utulivu katika maeneo yalioathiriwa na mashambulizi ya ugaidi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Lazarus Chakwera pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Namibia Dkt. Fredrick Shaba kabla ya kuanza kwa mkutano wa Dharura wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit). Januari 11,2022 Lilongwe Malawi.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akishiriki katika mkutano wa Dharura wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit) pamoja na Jamhuri ya Msumbiji na nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji. Januari 11,2022 Lilongwe Malawi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...