Na Khadija Seif, Michuzi TV
WAJASIRIAMALI na Wafanyabiashara nchini waaswa kutumia Mitandao ya kijamii Ili kujenga Mahusiano Mazuri na wateja wao pamoja na kutangaza biashara Kwa ujumla
Akizungumza na Michuzi TV Muasisi wa Kikundi cha Kusaidia wanawake katika ujasiriamali (Rich Women Forever)ambae pia ni Mmiliki duka la nguo watoto Abby Kids, Amina Ntomola amesema katika biashara yoyote ni muhimu kuwepo Kwa Matangazo na Wafanyabiashara kutumia Mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram pamoja na Whatsapp kuhakikishia wanajitangaza na kutangaza biashara zao kwani ina wafuasi wengi Kwa Sasa .
"Mitandao mara nyingi imekua ikitupatia wateja na itategemea utumiaji wa Mfanyabiashara mwenyewe lakini Kwa namna Moja au nyingine Mitandao imekua ikichangia Kasi ya kukua Kwa biashara na wafanyabiashara Kwa njia ya kujitangaza na kupelekea watu kuwafahamu au kufahamu biashara zao."
Hata hivyo Amina amewasihi wafanyabiashara kujikita katika kupata Elimu zaidi ya kibiashara Ili kuona Kwa jinsi wanaweza kukuza ,kupanua biashara kwani wengi wao hawapati Elimu ya kukabiliana na biashara,bidhaa gani ziletwe Kwa wateja ambazo wanaohitaji pamoja na swala la Mitaji.
"Nilipitia changamoto ya kuanza biashara nikiwa na Mtaji Mkubwa lakini nilijikuta nikipata hasara kutokana na kuweka mzigo mkubwa ambao Mahitaji yake sio makubwa dukani hivyo wafanyabiashara tukipatiwa angalau Elimu ya kukabiliana na biashara tutaweza kutengeneza biashara zenye Manufaa sio hasara hata Kwa Mitaji midogo midogo na sio lazima Kila Mfanyabiashara aweze kwenda kufata Mizigo china na sehemu zingine za nje ".
Pia amefafanua Kwa mwaka huu kundi la (Rich Women Forever) wamejipanga kutoa Elimu Kwa wajasiriamali hususani wanawake Ili waweze kufanya biashara zao Kwa weledi unaotakikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...